MURJI KUTETA NA WAANDAMANAJI KESHO

1178[1]MBUNGE wa Mtwara mjini Hasnain Murji kesho saa Tisa alhasiri anatarajia kukutana na viongozi wa umoja wa vyama vya siasa vilivyoungana kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam.

Vingozi hao ndiyo walioratibu maandamano Alhamisi Desemba, 27 mwaka huu na kukusanya maelfu ya wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Mbunge huyo, Meckland Millanzi tukio hilo litafanyika ukumbi wa kanisa la Pentekosite mjini Mtwara ambapo pia waandishi wa habari wamealikwa.

Millanzi hakuweza kuzungumzia ajenda za kikao hicho ila kwa mujibu wa Murji mwenyewe kikao hicho kitajadili zaidi namna ambayo wana Mtwara wanaweza kufaidiaka na gesi hiyo.

Mwisho

 

Advertisements