MTWARA WAMJIBU JK, WASEMA HAJASOMEKA

4

1

5

2

3
UMOJA wa vya tisa vya siasa vilivyoungana mkoani Mtwara vimesema msimamo wao upo palepale licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa msimamo wa suala hilo.

Wakihutubia katika mkutano wa adhara viongozi wa umoja huo kwa nyakati tofauti walisema hawako tayari kuiona rasilimali za nchi zikiendelea kusababisha umaskini kwa wananchi badala ya kuwakombo.

“Ukicheka na nyani utavuna mabua, wenzetu kwenye madini walicheka nao na wamevuna mabua, sisi hatuko tayari…tunatambua kuwa mamlaka ya nchi yapo mikononi mwetu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania…kama Kikwete amesema kwa namna yeyote ile gesi itatoka basi sisi tunamwambia kwa namna yeyote ile gesi hatoki” alisema Mohamedi Salim mjumbe wa umoja huo kutoka NCCR Mageuzi

Aliongeza kuwa “Kwanza tunataka Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo aondolewe katika wadhifa huo kwa sababu analeta propaganda za kisiasa kwenye masula nyeti yanayohusu maisha ya watu”

Kwa pande wake mwenyekiti wa Chadema wa wilaya ya Mtwara mjini, Mustafa Nchia alisema wataandamana hadi serikali itaposikia kilio chao, na kwa kuanzia wanataka Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Joseph Simbakalia aondolewe mkoani hapa kwa madai aliwatusi wananchi kwa kuwaita wapuuzi.

“Tulimpa siku 14 awe ameondolewa, leo bado siku tano… baada ya hapo tuitaandamana kumtaka aondolewe huku madai yetu ya msingi yakibaki palepale…pia tutamshitaki kwa kutuita sisi wahaini” alisema Nchia
Naye Makamu mwenyekiti wa Umoja huo Uledi Abdallah aklimpongeza mkuu wa polisi mkoani hapa (Maria Nzuki) kwa kuruhusu maandamano hayo na kuwataka wananchi kuondoa woga katika kusimamia rasilimali yao ili mradi wasivunje sheria.

“Tunampongeza RPC kwa kuruhusu maandamano, ndiyo askari tunaowahitaji kwa sasa…wito wangu kwa wananchi kuweni macho na rasilimali yenu, msiogope kudai haki yenu kwa sababu hakuna sheria tunayovunja…gesi yenyewe haina sheria wala sera’ alisema Uledi

Licha ya mvua kunyesha, bado mkutano huo uliendelea na hatimaye kukamilika kwa wananchi hao kuuchangia fedha umoja huo ili uendelee na mikutano ya kuhamsisha wananchi kulinda rasilimali yao ya gesi asilia.

Mikutano hiyo itaendelea kesho katika viwanja vya bima na kesho kutwa katika viwanja vya Nkanaledi.
Mwisho