RC MTWARA ADAIWA ‘KUHONGA’ WAZEE

1

Hata wanawake tumo

Hata wanawake tumo

3MKUU wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia anadaiwa kufanya kikao cha siri na baadhi ya wazee wa Mjini Mtwara kuwashawishi wakubaliane na msimamo wa serikali wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam ikitokea Msimbati mkoani Mtwara.

Katika kikao hicho kinachodaiwa kufanyika nyumbani kwake Mkuu wa Mkoa mbali ya kuwakirimu kwa chakula pia anadiwa kuwafa fedha sh. 50000 kila mmoja ikiwa ni sehemu ya shukurani zake kwa kuitika wito huo.

Mustafa Nchia ni mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Mtwara amewaambia wananchi katika mkutano wa adhara wa kupinga gesi kwenda Dar es Salaam uliofanyika eneo la Bima mjini Mtwara.

“Tunayo ushahidi, tunawafahamu wazee waliokwenda huko, walilipwa sh. 50000 kila mmoja ili atakapokuja rais waende kumwambia wana Mtwara tumekubali gesi iende dar es Salaam” alisema Nchinia.

Mbali na shutuma hizo, pia umoja wa vyama hivyo ulimtupia makombora mkuu huyo wa mkoa kwa kusababisha hasara ya zaidi ya sh. 800 milioni kwa kuamrisha kufungwa kwa Maisha Klabu.

Mwishoni mwa mwaka jana Maisha Klabu ilifungiwa na Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa madai ilikiuka taratibu za uanzishwaji wake.

Kufuatia hali hiyo suala hilo lilifuikishwa Mahakama Kuu ya Biashara na kuamriwa kufunguliwa kisha kumlipa fidia ya zaidi ya sh. milioni 800 kwa kumsababishia hasara.

“Tunayo ushahidi Simbakalia ndiye aliyeamrisha kufungwa kwa Maisha Klabu, leo halmashauri yetu inadaiwa zaidi ya sh. 800 milioni kwa uzembe wake…tunasema hatumtaki, aondoke” alisema Uledi Abdallah

Akizungumza na KUSINI Simbakalia aliahidi kuweka mambo hadharini hapo kesho Jumanne Januari, 8, mwaka huu.
Mwisho

Advertisements