MUHONGO NJOO MTWARA TUKUELIMISHE

Mustafa Nchia Mwenyekiti Chadema Mtwara

Mustafa Nchia Mwenyekiti Chadema Mtwara

UMOJA wa vyama Tisa vya siasa mkoani Mtwara umemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Spspeter Muhongo kuacha kulumbana kupitia vyombo vya habari na badala yake aende mkoani Mtwara ili wananchi wapate fursa ya kumuelimisha juu ya madai yao.

Kauli ya umoja huo imetolewa jana (leo) na Makamu Mwenyekiti, Uledi Abdallah akijibu shtuma zilizotolewa na Waziri Muhongo kwa vyama hivyo katika kupindi cha Dakika 45 kilichorusha na luninga ya ITV jana usiku.

Katika mazungumzo yake Muhongo aliwashtumu kuwa viongozi wa umoja huo mambumbumbu na kwamba wanasukumwa na dhamira za kisiasa badala ya uhalisia katika kujadili suala la mradi wa kusafirisha gesi kutoka Msimbati mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam kwa njia ya bomba.

Uledi aliiambia KUSINI amesikitishwa na kauli ya waziri huyo na kwamba anatilia shaka na usomi wake kwa madai kuwa bado hajaelimika na kumtaka afike mkoani Mtwara ili wananchi wamuelimishe.

“Kwanza aache malumbano ya kwenye TV, Magazeti na Redio, Mtwara sio mbali aje ili wananchi tumuelimishe kwasababu huenda amesoma ila bado hajaelimika…kama hana nauli atuambie tumchangie” alisema Uledi

Aliongeza kuwa “Unapopewa hoja inakupasa ujibu hoja si kumshambulia aliyetoa hoja, hii ni ishara kuwa huyu waziri hajaelimika, tuna mashaka na usomi wake…sisi tumeweka hoja tisa mezani ikiwemo ya kukataa kujengwa kwa vinu vya kufua umeme Kinyerezi jijini Dar es Salaam, kwa msomi kama yule tulitaraji ajibu hoja sio kutushambulia”

Alidai kuwa kauli anazozitoa inaonesha wazi si zake bali ameandaliwa na watu wengine ndiyo sababu ya kushindwa kuchambua na kujibu hoja.
“ Alisema saa hizi Dunia inategemea, gesi ya Afrika Mashariki, aliitaja nchi ya Msumbiji na Somali kama ni miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki, hii inaonesha wazi usomi wake unamashaka maana waziri huyu hajui hata Afrika Mshariki inaundwa na nchi gani..kama gesi Mtwara ni asilimia 14 kwanini basi watumie fedha nyingi kusafirisha gesi kidogo?” alidai Uledi

Mwisho

Advertisements