HOTUBA, NUKUU ZA NYERERE ZACHOCHEA MOTO WA GESI MTWARA

Hatutaki gesi iende dar

Hatutaki gesi iende dar

Mwenyekitiwa vijanaCUF taifa Katan Ahmadi Katani

Mwenyekitiwa vijanaCUF taifa Katan Ahmadi Katani

Tunachangia fedha za maafa ya mafuriko

Tunachangia fedha za maafa ya mafuriko

Nachangisha fedha za marufiko Mtwara, ni Katani Katani mwenyekiti wa vijana CUF Taifa.

Nachangisha fedha za marufiko Mtwara, ni Katani Katani mwenyekiti wa vijana CUF Taifa.

Mzee Rashid Kilembwend. nawaasa vijana lindeni gesi

Mzee Rashid Kilembwend. nawaasa vijana lindeni gesi

Saidi Kulaga Nyerere alisema hivi, Katibu wa CUF Mtwara mjini

Saidi Kulaga Nyerere alisema hivi, Katibu wa CUF Mtwara mjini

SAKATA la wakazi wa mkoa wa Mtwara kupinga rasilimali ya gesi asilia inayovunwa katika kijiji cha Msimbati mkoani humo kupelekwa Da es Salaam kwa njia ya bomba limepamba moto huku viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) wakitumia hotuba na nukuu za kauli za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuhamasisha wananchi kumuenzi mwasisi huyo wa taifa kwa kuupinga mradi huo.

Katika mkutano mkubwa uliofanyika jana Mtaa wa Sinani mjini hapa viongozi wa CUF wilaya ya Mtwara Mjini, walikuja na mbinu mpya ya kuhamsisha wananchi kuendelea na msimamo huo kwa kutoa hotuba na nukuu za kauli za Baba wa Taifa kuhusu mustakabali wa hali ya maisha ya wananchi katika mazingira ya wachache kuwakandamiza wengi.

Saidi Kulaga Katibu wa CUF wilaya ya Mtwara mjini, alisema kinachotokea leo kwa wakazi wa mikoa ya kusini ni kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ambaye kwa nyakati tofauti alinukuliwa akionya viongozi kugandamiza wengi.

Katibu huyo akiwa anasoma karatasi ya nukuu hizo kutoka kitabu cha ‘Reflection on Leadership in Africa’ kilichopigwa chapa na VUB University Press, 2000 alisema mwasisi huyo wa Taifa katika kitabu hicho amenukuliwa akisema

“Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala, mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wanapoteza matumaini na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?”

Akiendelea kusoma nukuu hizo alisema “Amani ni zaola matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii…Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi, kwanini wasiasi?…Pale wananchi wengi wanapopoteza matumaini inajengeka volcano, volcano ambayo siku moja italipuka, labda kama watu hawa ni wajinga.”

Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu Kulaga alisema “Sio mimi ni Mwalimu Nyerere anasema….wengi katika nchi zetu ni wajinga ndiyo maana wanakubali kutawaliwa hivyo, kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa sababu ya ujinga tu, hivyo basi watanzania watakuwa wajinga na matahira (idiots) kama watakubali kuendelea kukandamizwa na kikundi cha wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe”

Katibu huyo alisema Nyerere katika kitabu hicho anasema“Ni ukweli usiopingika kuwa masuala ya maendeleo hayawezi kuwa masuala ya ubabaishaji tu na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku chache zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao (wananchi) na watoto wao wakiendelea kuishi maisha duni na dhalili”.

Alibainisha kuwa kwa kuwa Serikali imeshindwa kuyaenzi maneno ya Mwalimu Nyerere wakazi wa Mtwara wamejitolea kuyaenzi maneno hayo kwa vitendo na kwamba hakuna tonela gesi ghafi itakayosafirishwa kwa njia ya bomba hadi Dar es Salaam.

Alifafanua kuwa wananchi wanatambua wazi kuwa gesi ni rasilimali ya
Taifa lakini alihoji kwanini Twiga wanaopatikana katika hifadhi za Serengeti hawahamishiwi katika hifadhi za kusini, ili hali ni rasilimali ya Taifa?

“Naomba Tueleweke hatupingi gesi kunufaisha Taifa ila tunapinga mitambo ya kufua umeme kujengwa Dare s Salaam tunataka mitambo na viwanda vijengwe Mtwara halafu faida itakaopatikana ilinufaishe Taifa” alifafanua Kulaga

Katibu huyo pia aliweka hotuba ya Nyerere mkutanoni hapo inayopinga matumizi mabaya ya rasilimali zanchi kwa kunufaisha wachache huku wengi wakiendelea kuteseka, kitendo hicho kilivuta hisia za wengi.

Mwenekiti wa Jumuiya ya Vijana wa CUF Taifa, Katani Katani alisema uvumilivu wa watu wa kusini wa kudhulumiwa fursa za maendeleo umefika mwisho na kwamba hawako taari kuona gesi asilia ambaye aliifananisha kuma karata ya mwisho ikishindwa kuwakomboa.
“Tushikamane kwa hili, tuweke tofauti zetu kado…tuiambie seikali

katika hili hapana…kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya salamu za mwaka mpya amesema lazima gesi itaondoka basi tunamweleza haiondoki ajiandae kwa hatua nyingine” alisema Katani huku akishangiliwa na vijana.

Tofauti na mikutano mingine mkutano huo ambao uliitishwa na CUF pekee, ulihutubiwa pia na kada wa CCM, Mzee Rashid Abdallah ambaye aliwataka vijana kuwa msitari wa mbele kutetea maisha yao.

“Hii gesi siyo ya kwetu sisi wazee, uliwahi kusikia maisha yanatafutwa uzeeni, tunataka gesi ibaki kwa ajili yenu na watoto wenu….simamieni” alisema Mzee Abdallah huku akishangiliwa kwa nguvu na wananchi waliofurika mkutanoni hapo.
Mwisho

Advertisements