WAISLAM MTWARA: TUTAPIGANA JIHADI KUTETEA GESI

Sheikh Jamalidini

Sheikh Jamalidini

Mambongo yalikuwapo

Mambongo yalikuwapo

Tunaswali

Tunaswali

DSCN1970

Tunakunuti

Tunakunuti

WAUMINI wa Dini ya Kiislamu mkoani Mtwara jana wametoa tamko nzito la kupinga gesi asilia inayovunwa kijiji cha Msimbati, mkoani humo kupelekwa Dar es Salaam kwa njia ya bomba na badala yake wameitaka serikali kusitisha mpango huo ili kunusuru hali tete ya kiusalama inayoweza kutokea.

Katika mkutano huo uliofanyika Viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara na kuudhuriwa na maelfu ya watu, waislam hao walizindua kaulimbiu mpya ya ‘gesi kwanza, uhai baadae’ kaulimbiu ambayo inatoa ishara mbaya iwapo jitihada za kumaliza mzozo huo hazitafikiwa mapema.

Akisoma tamko la Shura ya Maimamu wa mkoa wa Mtwara Ustadhi Mohamedi Salumu alisema waislam hao wameamua kuungana na wananchi wote wa Mtwara wanaopinga mradi huo kwa maelezo kuwa hauna faida kwa wakazi wa mkoa huo na Lindi.

Alisema waislam mkoani humo wapo tayari kutetea rasilimali hiyo ili isisafirishwe ghafi kwenda Dar es Salaam hata ikibidi kumwaga damu na badala yake mitambo ya kuchakata na kufua umeme ifungwe Mtwara na kwamba zao la mitambo hiyo inaweza kushafirishwa kokote nchini.

Kabla ya kutolewakwa tamko hilo waislam walifunga kwa siku saba mfululizo tangu Ijumaa ya wiki iliyopitahuku wakisoma kunuti (dua maalum) ya kumuomba MwenyeziMungu afanikio kusidio lao la kupinga gesi kwenda dare s Salaam, dua ambayoilihitimishwa uwanjani hapo.

“Waislam tumesema basi inatosha…mambo mengi kusini tumedharauliwa, bandari imekufa, barabara haijajengwa, reli imeng’olewa, taa za uwanja wa Ndege zimeng’olewa na kupelekwa Arusha…tunaishauri serikali isitishe mradi huo…maana panapokuwa na sikubali mbili mwishowe ni ugomvi” alisema ustadhi Salumu

Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu alifafanua kuwa “Hili suala si la kisiasa, tatizo lingekuwapo hata kama wanasiasa wasingekuwapo…tunadai haki zetu..kupinga gesi kwenda Dar es Salaam sio ujinga…tunaiomba serikali hata kama haiwapendezi hoja hii wasipotoshe ukweli, wajibu hoja kama ilivyosimama…gesi kwanza?” alihoji…uhai baadae”wananchi walijibu

Masheikh mbalimbali walihutubia waumini na wananchi walioudhuria kongamano hilo kwa kutoa kauli ambazo inaashiria mzozo huo kushika kasi huku kukiwa na kila dalili za kuvunjika kwa amani iwapo serikali haitakaa chini na wananchi hao.

Sheikh Jamadini Mchamwi alisema hadi sasa serikali haijajibu hoja ya wanaMtwara badala yake imekuwa itoa kauli za vitisho jambo ambalo alisema halimalizi mzozo uliopo bali kuendelea kupandikiza chuki kwa wakazi wa kusini.

“Mimi sidhani serikali itatupeleka huko wanakotaka tufike…hatutafuti mshindi hapa…ni vema serikali ikanusuru giza lililopo mbele…ikubali hasara za hizo trilioni Tatu…tumepata hasara matrilioni mangapi sembuse hizi…hakuna fedha yenye thamani na maisha ya watu…kwanini tusimalize mzozo kabla ya roho za watu kuteketea, hakuna sifa ukiua” alisema Mchamwi na kuongeza

“Kikwete asitafute kuua watu kwa sababu ya kupinga gesi…naomba sana viongozi wetu wasimpe shetani nafasi…tuwaombee dua viongozi wetu wamjue Mungu…viongozi wetu wamekosa hoja katika hili…waislam imefika wakati tunasema basi, gesi haitoki…mwambieni asitake kumaliza vibaya uongozi wake”

Naye Sheikh Hussein Mchomola kutoka wilaya ya Masasi alisema hoja inayotumiwa na viongozi wa serikali ya kuikana Mtwara kuwa sio sehemu ya Tanzania na kwamba wanunuzi wa gesi hawawezi kufika inaweza kulifikisha pabaya Taifa.

“Kama mnunuzi atakuaja kwa Ndege uwanja tunao, kama mnunuzi atakuja kwaBoti, bandari tunayo na kama atakuaja kwa gari maliza barabara…kuna ubaya gani vinu vya kufua umeme vikibaki Mtwara, viwanda vikajengwa Mtwara, kwani huku sio Tanzania?” alisema Mchomola huku akishangiliwa na wananchi

Sheikh Mohamedi Makombo kutoka Msimbati ambako gesi asilia inachimbwa alisema wanakijiji hao hawapo tayari kuiona gesi yao ikisafirishwa gafi na kwamba wapo tayari kwa lolote.

“Tumesema hatukubaliani kwa hili, na vijana wamenituma niwaambie kuwa wao wapo tayari, hawaogopi kufa kwa kuwa kila mmoja ataonja mauti, ila kwa sababisho tofauti” alisema

Tamko hili linaungana na lililowahi kutolewa na Askofu Mteule wa KKKT kanda ya Kusini Mashariki, Mchungaji Lucas Mbegule na Askofu wa Kanisa la Angalikana Dayosisi ya Newala, Oscar Mnung’a na hivyo kuiondoa hoja ya kiasa katika mzozo huo.
Mwisho

Advertisements