MAELFU MTWARA WAPINGA GESI KWENDA DAR

3

MAELFU ya wakazi wa mkoa wa Mtwara wamejiandikisha katika fomu maalum za kupinga gesi asilia inayovunwa kijiji cha Msimbati mkoani humo, kupelekwa Dare s Salaam.

Tayari majina hayo yamekabidhiwa kwa Katibu wa Wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) Magdalena Sakaya kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni kama kielelezo halali cha wananchi hao kupinga mradi huo, utaratibu wa kujiorodhesha uliandaliwa na chama hicho.

Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya mkutano mkubwa wa adhara uliofanyika viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara na kuudhuriwa na maelefu ya watu kutoka wilaya zote tano ya mkoani hapa.

Mashuhuda wa mkuatano huo wanasema haijawahi kutokea umati mkubwa wa watu kuudhuria mkutano, wakilinganisha na maandamano ya Desemba, 27 mwaka jana ya kuupinga mradi huo na ziara mbalimbali za viongozi wa kitaifa.

Majina hayo yalikabidhiwa na makatibu wa CUF wa kila wilaya huku mwenyeji wao, Saidi Kulaga alisema zaidi ya watu 30,000 wamejiandikisha ikiwa ni kielelezo tosha cha wananchi hao kupinga gesi ghafi kusafirishwa na badala yake wanaitaka serikali kujenga mitambo ya kufua umeme na kuchakata gesi mkoani humo ili kuinua uchumi wa mikoa ya kusini.

“Kwa niaba ya wananchi hawa nakukabidhi mbele yao majina, makazi na sahihi zao wakipinga mradi wa kusafirisha gesi ghafi kwenda Dar es Salaam…wananchi hawa wanasema gesi haitoki ng’o…wamejipata kutetea rasilimali yao…wazee wetu waliwaondoa wanyonyaji weupe sasa ni zamu ya vijana kuwaondoa wanyonyaji weusi” alisema Kulaga huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Akipokea fomu hizo Sakaya alisema wao kama wabunge wamesikia kilio cha wananchi wa Mtwara na watahakikisha wanawasilisha kwenye Bunge lijalo.

Licha ya kunyesha mvua kadri muda ulivyosonga mbele ndivyo watu walivyozidi kuongezeka, maduka na soko kuu lilifungwa saa 8. Mchana ili kutoa fursa ya wafanyabishara na wananchi wengine kushirki katika mkutano huo mkubwa wa kihistoria.

Kabla ya mkutano kuanza umeme ulikatwa katika eneo hilo la mkutano hali iliyosababisha kundi la vijana kuivamia ofisi ya Tanesco mkoani hapa wakiishinikiza kurudisha umeme, kitendo kilichowalazimu polisi kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi hao.

Wananchi waliondoka eneo la ofisi za Tanesco na kurudi uwanja wa mkutano na baadae kidogo umeme ulirudi hali iliyotoa fursa kwa mkutano huo kuendelea kwa amani na utulivu huku polisi muda wote wakiwa katika taadhari kubwa.

Mwenyekiti wa Vijana Taifa wa CUF Katani Katani alitoa taarifa mkutanoni hapo kuwa moja ya gari lililokuwa limebeba wananchi kutoka Tandahimba kwenda kwenye mkutano huo limepinduka na watu kadhaa wamejeruhiwa na hakuna aliyepoteza maisha.

“Mwambieni Kikwete (Rais Jakaya) wananchi wa kusini hawataki gesi yao iende dare s Salaam na kama atabisha basi ajiandae kuua wananchi….tumesema baasi inatosha…gesi inatoka haitokiii” aliuliza katani na wananchi kumjibu “Haitokiii”

Pia katika mkutano huo mabango kadhaa yalibebwa na baadhi yalisomeka “Shemejiii gesi haitoki….Kikwete tuachie gesi yetu”

Kabla ya kutoa hotuba yake Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro aliwalisha kiapo wananchi na viongozi walioudhuria mkutano huo, cha kutosaliti maamuzi ya mkutano na kutorudi nyuma na kwamba wote watakaokwenda kinyume laana za mungu ziwafikie.

“Katibu wa wabunge na wabunge wote wa CUF nawaagiza hakikisheni haoja hii ya wananchi munaifikisha Bungeni na munaitetea, vinginevyo chama hakitawaelewa…makamanda na majanki mpooo? Alisema Mtatiro huku mvua kubwa ikimnyeshea mwilini baada ya kukataa mwavuli.

Tukio hilo loinatokea wakati jana waislam wamefanya dua maalum ya kumuomba Mwenyezi Mungu kutia wepesi hoja yao ya kutaka gesi ibaki Mtwara na kuwalaani wale wote wanaotaka rasilimali hiyo iondoke.

mwisho

Advertisements