SAKATA LA GESI SASA LAWASHUKIA WABUNGE

Hata wanawake tumo

Hata wanawake tumo

SIKU moja baada ya wananchi zaidi ya 30,000 wa mkoa wa Mtwara kusaini katika fomu maalum za kupinga gesi ghafi kusafirishwa Dar es Salaam na kuzikabidhi kwa wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), umoja wa vyama Tisa vya Siasa vilivyoungana mkoani hapa kuipa nguvu hoja hiyo umemuomba Rais Jakaya Kikwete kukumbuka usemi wa ‘Mafahali wawili hawakai zizi moja’ hivyo wamemtaka kutumia busara kusitisha mradi huo ili kuepusha uvunjifu wa mani unaoweza kujitokeza.

Pia umoja huo umewataka Wabunge wote wa mkoa wa Mtwara kila mmoja kutangaza msimamo wake juu ya kuunga mkono hoja ya wananchi ya kukataa gesi ghafi kwenda Dar es Salaam au kukubaliana na uwamzi wa Serikali ili wananchi wajue ni Mbunge gani msaliti kwao.

Wakizungumza katika mkutano wa adhara uliofanyika jana (leo) katika uwanja wa Sabasaba mini hapa, viongozi hao kwa nyakati tofauti wamemtaka Rais Kikwete kutotumia jazba na mabavu katika kulipatia suluhu jambo hilo na badala yake busara zitawale kwa kusitisha mradi huo.

“Sisi Watanzania hatujazoea vita, ila tumezoea kupata hasara…katika hili naomba Kikwete akubali kupata hasara kama tunavyokubali hasara zingine…sisi wananchi tupo radhi tuingie kweny deni kubwa kama hilo, lakini gesi haiwezi kwenda Dar es Salaam” alisema Uledi Abdallah Makamu mwenyekiti wa umoja huo

Aliongeza kuwa “Hizo trilioni tatu kama Anaona hawezi kuzilipa iwapo gesi itabakia Mtwara…basi atafute njia zingine za kulilipa…atambue kuwa hakuna fedha yenye thamani ya amani na utulivu wetu…akumbuke kuwa mafahali wawili hawakai zizi moja”

Naye mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Mtwara Mjini, Mustafa Nchia aliwataka wabunge kutoa misimamo yao ili wananchi wajue ni mbunge yupi anawaunga mkono na yupi mslaiti kwao.

“Hadi sasa ni Hawa Ghasia (Mtwara vijijini), George Mkuchika,(Newala), Asnain Murji(Mtwara Mjini) na Clara mwatuka (Viti maalum CUF), wametoa misimamo yao, vipi ninyi wengine…tunataka kusikia msimamo wa kila mmoja” alisema Nchia huku akishangiliwa na mamia ya watu walioudhuria mkutano ho

Alisisitiza kuwa “Waislamu wametoa tamko lao, tunasubiri la wakristo, na kila kundi katika jamii tunahitaji misimamo yao, hatufanyi mzaha kwenye kutetea rasilimali yetu…wananchi wanataka kujua nani msaliti wao”

Mwisho

Advertisements