ZITTO:UKOMBOZI HAUJI KWA LELEMAMA, MSIKATE TAMAA MTWARA

Zitto Kabwe

Zitto Kabwe

MBUNGE wa Kigomba Kusini, Zitto Kabwe amewataka wakazi wa mikoa ya Kusini kutokata tama katika mapambano ya kujikomboa kutokakwenye miaka 51 ya ufukara kwa kupinga kusafirishwa kwa gesi asilia inayopatikana Msimbati mkoani Mtwara.

Akizungumza na Info Redio ya mjini Mtwara, Zitto alisema licha ya serikali kutumia vitisho bado hawapaswi kurudi nyuma kwa kuwawananchi hao wameanzisha vuguvugu la ukombozi wa kiuchumi nchini.
Kwa kauli yake Zitto ambaye pia ni Naibu katibu Mkuu wa Chadema Taifa anasema.

“Naungana na wananchi wa mtwara katika kutetea raslimali yao ya gesi asilia na serikali inatakiwa kuwasikiliza wananchi wa Mtwara kuhusu madai yao haya ya kutoondolewa kwa gesi na sio kuwabeza na kuwaita wahaini”…

Kuna ulazima gani wa gesi kusafirishwa na kuletwa Dar es salaam badala ya kujenga kinu cha kuchakata umeme na gesi Mtwara? huku ni kutumia mamilioni ya pesa ambayo yangeweza kuendeleza mambo mengine ya msingi.”

Wananchi wa Mtwara hawakatai gesi kusafirishwa lakini wanachotaka wanuafaike nayo kwanza ndipo raslimali hiyo ya taifa iwanufaishe watanzania wengine.

Serikali ni kweli inaweza kuwaweka askari hata huko porini ambako bomba hilo litapituishwa? Msikate tama ndugu zangu wa Mtwara, kazeni buti safari ya ukobozi bado ni ndefu.
Mwisho

Advertisements