KIKWETE KUTUA MTWARA

Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete

HABARI zilizoifikia KUSINI hivi punde zinaeleza kuwa Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuwalisi mkoani Mtwara Januari, 29, mwaka huu siku ya Jumanne kushughulikia suala la gesi.

Kikwete akiwa mkoani Mtwara inadaiwa atafanya kikao na wazee wa Mtwara, naalitarajia kuonana na Bibi Mtiti, Mkuu wa kaya ya Msimbati ambako gesi inachimbwa.

Hata hivyo kumekuwapo na mvutano kutokana na baadhi ya maofisa usalama kumshauri asije kwa wakati huu kwa kuwa jazba za wananchi wa Mtwara bado haijapoa.

“Kikwete atakuja Jumaane ijayo…lakini wapo watu wanamshauri asije kwa sasa” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina

Habari hizo zinashabiana na zile zilizodokezwa na Seleman Babu mtu anayedaiwa kuwa ni Mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye alkwenda msimbati kutengeneza mazingira ya Bibi Mtiti kukutana na Rais Kikwete siku ya Jumanne mjini Mtwara.
Mwisho

Advertisements