MAUAJI, MAUJI MASASI, SABA WAUAWA

WATU Saba akiwemo askari polisi mmoja wameuawa katika vurugu zinazoendelea wilayani Masasi mkoani Mtwara, zikiwazimebebasura ya kupinga gesi kwenda Dar es Salaam.

Muuguzi wa zamu hospitali ya wilaya ya Masasi, Mkomaindo Fatuma Timbu amethibitisha kupokea maiti za watu saba.
Majeruhi ambao idadi yao haijajulikana wamekimbizwa hospitali ya misheni ya Ndanda kwa matibabu na hali bado ni tete.

Vurugu kubwa zilianza majira yasaa 4 asubuhi baada ya polisi waliokuwa wakiendesha pikipiki kumgonga mtu na kukataa kutoa ushirikiano

Hata hivyo hoja hiyo ilihamia kwenye gesina kundi la viajana mara moja walivamianyumba ya mbunge wa Masasi, Mariam kasembe na kuiwasha moto, pamoja na magari mawili.

Pia vijana hao walivamia nyumba ya Anna Abdallah na kuiteketeza kwa moto,kabla ya kuivania ofisi ya CCM wilaya na kuichoma mot pamoja na magari matatu.

Hasira za wananchi hao zilifika kituo kidogo cha polisi kilichopo Mkuti na kukichoma moto, baadaewalichoma moto magari matano ya halmashauri ya wilaya.

Pia walichoma moto ofisi ya elimu ya halmshauri ya wilaya Masasi vijijini, kabla ya kuichoma ofisi ya maliasili joni hii.

Polisi kutoka maeneo mbalimbali yandanina nje ya mkoa inadaiwa walitumia risasi za moto na kusababisha vifo vya watu Sita huku polisi akidaiwa kuuawa kwa kupigwa na wananchi….
Endelea kuifutilia KUSINI