MTWARA HAKUNA KUTOKA WALA KUINGIA

2

MTWARA sasa hakuna kutoka wala kuingia, Mhariri Mtendaji wa KUSINI ameshuhudia hali hiyo saa 11 alfajiri katika barabara zote mbili zinazoingia na kutoka Mjini Mtwara.

Barabara iendayo Tandahimba, hadi Newala eneo la Magomeni stendi ya Newala kwa mbele kidogo barabara imefungwa kwa magogo na mawe, pia kuna kudni la vijana wenye siala za jadi yakiwemo mawe wamekesha kulinda kizuizi hicho.

Barabara ya kwenda Dar es Salaam nayo ni mbaya zaidi kwa sababu katika eneo la Mkanaledi kuna vizuizi vitatu vya magogo na mawe, pia kizuzi kikubwa kipo eneo la pacha ya kwenda Mbaye ambapo kuna kundi la vijana lililokesha kuhakikisha hakuna anayeingia wala kutoka ndani ya mji huo.

Hizo ndiyo barabara kuu za kuingia na kutoka Mjini Mtwara…endelea kuifuatilia KUSINI kwa matukio zaidi

Advertisements