MURJI KUNYANG’ANYWA KADI YA CCM TENA

MURJI[2]HABARI za kuaminika kutoka vyanzo vyetu vya habari ndani ya CCM Taifa zinaeleza kuwa Mbunge wa Mtwara Mjini Asnain Murji anaweza kunyang’anywa kadi ya uwanachama wa CCM mda wowote kuanzia sasa kwa madai alichochea vurugu za wapinga gesi.

Habari zinasema kuwa tayari CCM mkoa wa Mtwara imependekeza hatua hiyo kama kafara na fundisho kwa wabunge wengine wanaopinga mipango ya serikali ya CCM ili hali wao ni wabunge kupitia chama hicho.

“Murji atanyang’anywa kadi hivi karibuni…vikao vya CCM mkoa vimembainisha kama msaliti wa chama na kwamba alikuwa ‘ana fadhili’ vurugu zilizotokea Januari 25/6 mjini Mtwara na wilayani Masasi…yeye ndiye atakayetolewa kafara” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina.

Iwapo Murji atanyang’anywa kadi itakuwa mara ya pili kwa tukio hilo ambapo katika tukio la kwanz mwaka 2003 alinyang’anywa kadi ambayo alirejeshewa mwaka 2008 na hivyo kumwezesha kugombea ubunge.

Habari zaidi endelea kufuatilia KUSINI….

Advertisements