KINANA ATEMBELEA MTWARA KIMYAKIMYA

Kinana

Kinana

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abrahaman Kinana leo amefanya ziara ya ghafla mkoani Mtwara na kuzungumza na kamati ya siasa ya wilaya ya Mtwara Vijijini.

Kinana pia alitem,belea wilayani Masasi ambako alijionea mabaki ya ofisi ya chama hicho baada ya kuteketezwa kwa moto Januari 26 mwaka huu.

Habari ambazo hazina shaka zinaeleza kuwa pamoja na mambo mengine kiongozi huyo wa chama tawala alijaribu kuziba mpasuko unaodaiwa kukiweka chama hicho katika hatari kubwa ya kugeuzwa chama cha upinzani katika majimbo ya mkoa wa Mtwara.

“Ni kweli alifika kwa ziara ya ghafla..alikuja kuwapa pole waliopatwa na maafa hayo..ilikuwa ziara ya siku moja na ameondoka baada ya kuona hali halisi kule Masasi” alisema Alhaji Masoud Mbengula Katibua wa CCM mkoa wa Mtwara.

Mwisho