UMOJA WA VYAMA MTWARA WATETA NA PINDA

E81A4928UMOJA wa vyama Tisa vya Siasa vya upinzani mkoani Mtwara vinavyoongoza hoja ya wananchi wa mkoa huo kupinga mradi wa usafirishaji wa gesi kwa njia ya bomba hadi Dar es Salaam umekutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kumfikishia ujumbe kuwa wananchi wa Mtwara hawajamwelewa.

Kikao hicho kilifanyika nyumbani kwa Waziri Mkuu Pinda Jumamosi, 2 mwaka huu jijini Dar es Salaam baada ya umoja huo kukosa nafasi ya kukutana naye kwa mara ya pili wakati Pinda alipomaliza majumuisho Veta mjini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Mtwara, mmoja wa wajumbe wa umoja huyo Mustafa Nchia ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Mtwara mjini, alisema walilazimika kufunga safari kuonana na waziri mkuu kumfikishia ujumbe kuwa wananchi wa Mtwara bado hawajamwelewa.

“Tulikutana Jumamosi nyumbani kwake Dar es Salaam, tukamwambia kuwa wananchi wa Mtwara bado hawajakuelewa…yeye baada ya kumaliza majumuisho hakutuuliza kama tumekubaliana au laa…alikwenda kwenye vyombo vya habari na kusema amemaliza mgogoro” alisema Nchia

“Sisi tumemwambia bado wananchi wa Mtwara wana manung’uniko moyoni mwao, hanataka gesi isisafirishwe kwa njia ya bomba” aliongeza

Alieleza kuwa pia walimfikishia Waziri Mkuu Pinda, kilio cha Wana Mtwara cha kumkataa Mkuu wa Mkoa Joseph Simbakali kwa maelezo kuwa tayari watu wamekosa imani naye hivyo hawawezi kushirikiana vema katika maendeleo.

Simbakalia katika kikao cha majumuisho cha Waziri Mkuu cha Januari, 28 mwaka huu, aliwaomba radhi wakazi wa Mkoa huo kwa kuwaita wapuuzi na badae wahaini baada ya kumwalika kupokea maandamano Desemba, 27 mwaka jana.

“Tulimshauri Waziri Mkuu amuhamishe si tu kwa sababu watu wa Mtwara hawamtaki, lakini pia hata kama ataendelea kuwapo Mtwara watu hawapo tayari kumpa ushirikiano…ili afanye kazi vizuri na wananchi wa Mtwara wawe na hari ya kutoa ushirikiano kwa serikali yao ni vema akahamishwa” alisema Nchia

“Ametuhakikishia kulifika hili kwa Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa yeye ndiye aliyemteua…haya masuala mengine atujibu kuwa ametusikia”

Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Uledi Abdallah alisema pia walimuomba waziri mkuu awafungulie kuendesha mikutano ya adhara ili wananchi waweze kupata taarifa sahihi za mustakabali wa madai yao.

“Mtakumbuka kuwa kanda hii ya kusini kumezuiliwa mikutano ya kisiasa, sisi tumemwambia hapo hatatui tatizo bali anaongeza…tatizo la watu wa Mtwara hawapati taarifa sahihi kwa wakati na njia ya kuwapa taarifa hizo ni mikutano ambayo wametuzia…hapo tunaandaa tatizo lingine” alisema Abdallah

“Iwapo hatutaruhusiwa kuendesa mikutano, tutaandaa maandamano makubwa ambayo hata kama hatutapata kibali tutayafanya kudai haki yetu ya kueleza hisia na mawazo yetu, haki ya kupata na kutoa habari” alisisitiza.

Msemaji wa Umoja huo Hamza Masoud Licheta alisema kuwa si kweli kwamba umoja huo umehongwa fedha ulipokwenda kuonana na waziri mkuu bali ulikwenda kufikisha ujumbe sahihi wa watu wa Mtwara.

“Nataka niseme kuwa sisi hatukuitwa na waziri mkuu ila sisi tulimuomba kuonana naye baada ya kushindwa kuongea naye mara alipomaliza majumuisho…akatukubalia na ndipo tulipokwenda” alisema Licheta.

Licheta alitoa kauli hiyo baada ya kuwapo kwa madai kuwa viongozi wa umoja huo wameitwa dare s Salaam na waziri mkuu kwa lengo la kuwarubuni ili walegeze msimamo wao wa kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam

Mwisho

Advertisements