TAHLISO:DAWA YA WANAVYUO MAKAHABA IPO JIKONI

Katibu Mtendaji wa TAHLISO, Donati Salla.

UMOJA wa Serikali za Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO) imekiri kuwapo kwa baadhi ya wanafunzi wa kike wanaotumia mitandao ya kijamii kufanya biashara ya ngono na kwamba ‘dawa yao ipo jikoni’

Akizungumza na Mwananchi Jumapili mjini Mtwara, Katibu Mtendaji wa TAHLISO, Donati Salla alisema kupitia uchunguzi wa awali uliofanya na umoja huo katika mitandano ya twitter, facebook, BBM na Instagram umebaini kuwapo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini pamoja na makundi ya mitandao ya wanafunzi hao.

Katibu huyo alikuwa alijibu habari ya kiuchunguzi iliyochapishwa na gazeti hili wiki iliyopia, iliyobaini kuwapo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wanaotumia mitandano ya kijamii kufanya biashara ya ngono.

Februati 3 mwaka huu, gazeti hili lilichapisha habari iliyopewa jina la Ripoti Maalum, ikiwa imebebwa na kicha cha habari “Wanafunzi wa kike vyuoni watumia mitandao kujiuza” ikiwataja baadhi ya wanafunzi wa kike wa Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Dodoma, SAUTI, Elimu ya Biashara (CBE) na Taasisi ya Utawala wa Fedha (IFM) kuhusika na biashara hiyo.

“Sekretarieti imefanya uchunguzi wa awali juu ya uwapo wa mitandano na mtandao wa makundi ya wanafunzi wanaojishughulisha na ukahaba….tulifanikiwa kuwakuta katika mitandao iliyotajwa…TAHLISO sasa itafanya uchunguzi wa kina ili kupina ukweli wa taarifa hizi” alisema Salla na kuongeza

“Wale tutakaowakamata wakifanya vitendo hivyo vya aibu taarifa zitapelekwa katika vyuo vyao kwa hatua zaidi, uongozi wa TAHLISO utaangalia njia sahihi za kukabiliana na tatizo hili ikibidi njia za kisheria…pia nawaomba viongozi wa jumuiya za kidini za wanafunzi na vyuo kuchunguza katika maeneo yao na kubaini njia sahihi kukabiliana na tatizo hili ambalo linaharibu heshima ya vyuo vikuu nchini”

Akizungumzia wanafunzi walikosa mikopo kwa mwaka 2012/13, Salla alisema zaidi ya wanafunzi 1750 hawatapata mikopo hiyo.

Alisema baada ya mazungumzo ya kina baina ya Waziri wa Elimu na Mafunzo Dk. Shukuru Kawambwa,TAHLISO na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini ilibainika kuwa wanafunzi hao hawakufuata utaratibu wa kuomba mikopo hiyo kwama walivyoelekezwa.

“Walipaswa hukuisha maombi ya mikopo yao kwa njia ya mtandao kama walivyoelekezwa…kwa bahati mbaya hawakufanya hivyo, kwa hiyo imebainika kuwapa mikopo ni kinyume na utaratibu…hawatapata mikopo hadi hapo uwamzi mwingine utakapofikiwa na mamlaka husika” alisema

Alipokulizwa iwapo wanafunzi hao kukosa mikopo haoni kama inaweza kuchangia kushamiri kwa biashara ya ngono alisema “Wapo wanaopata asilimia 100 mkopo nab ado wanajiuza…hili ni suala binafsi…walipewa mda wa kutosha kabisa wa kuweza kuhuisha…ni uzembe wao”

Katika hatua nyingine TAHLISO imefanya uchaguzi Desemba, 16 mwaka jana na Januari 11 mwaka huu kupata viongozi wake wa kitaifa.

“Katika uchaguzi wa kwanza tulilenga kuwapata Sita wa umoja ambapo nafasi ya mwenyekiti ilichukuliwa na Amon Chakushemeire, Makamu Mwenyekiti Hamad Bakari, Donati Katibu Mkuu Mtendaji na Haji Rozzo naibu katibu mkuu mtendaji…wengine ni Ignatus Mponji Mweka Hazina na Mwamvua Shayo msaidizi wake”

Aliongeza kuwa “Uchaguzi wa pili ulilenga kumchagua mwenyekiti wa baraza la TAHLISO ambapo, Silasi Malima alishinda nafasi hiyo ambapo ataongoza kwa mwaka 2012/13 tu.
Mwisho

Advertisements