WAISLAM, WAKRISTO WAZICHAPA MWANZA

MGOGORO wa ckuchinga umeanza kulifikisha Taifa pabaya, ambapo habari za hivi punde kumezuka mapigano baina ya Waislam na Wakristo.

Tayari Misikiti kadhaa imechomwa moto na watu ambao idadi yao haijajulikana wamejeruhiwa na mmoja anadaiwa kupoteza maisha.

Mapigano hayo yanadaiwa kuchochewa na Wachungaji ambao jana walisema hawawezi kula nyama ilivyochinjwa na Muslamu, hivyo walitenga eneo lao kwa ajili ya kuchijia.

Asubuhi ya leo Wakristo hao walichinja wanyama kadhaa na kuanza kuu kwa wenzao, kitendo kilichosababisha baadhi ya waislam kuvamia eneo hilo na kuanza kufanya vurugu.

Habarui kutoka eneo la tukio zinasema kuwa pikipiki, mabajaji kadhaa yameteketezwa kwa moto, huku silaha za jadi zikitumika katika vurugu hizo.

Polisi wamewasili eneo la tukio na kuanza kurusha mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia hizo.
mwisho

Advertisements