WANAJESHI 3 WAFA AJALINI 23 WAJERUHIWA

Wanajeshi 3 wamekufa ajalini mjini Nachingwea mkoani Lindi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Nachingwea kwenda mkoani Mtwara kupinduka na wengine 23 kujeruhiwa

Habari za siri zinadai kuwa majeruhi wanakimbizwa katika hospitali za Ndanda na Nyangao kwa matibabu. Askari hao walikuwa wanakwenda Mtwara kusaidia kutuliza ghasia

Katika hatua nyingine Watu 45 wanashikiliwa na polisi kwa vurugu za kupinga gesi kwenda Dar es Salaam kwa njia ya bomba zilizotokea leo.

Kamanda wa Polsisi wa mkoa wa Mtwara Linus Sinzumwa amesema hakuna aliyekufa wala kujeruhiwa katika matukio yanayoendelea mjini hapa.

Kauli hiyo ya kamanda Sinzumwa inapinga nay a Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohamedi Kodi aliyethibitisha kupokea mwili wa mtu mmoja na wengine wengi kujeruhiwa.

Amesema kwa kiasi kikubwa jeshi lake limefanikiwa kutuliza ghasia na kwamba katika maeneo machache wanaendelea na kudhibiti hali hiyo.

Advertisements