SAKATA LA GESI, MBUNGE MTWARA MJINI MBARONI

11781Mbunge wa twara jinni Hasnein Murji (pichani) amekamatwa na polisi leo saa 11 jioni nyumbani kwake maeneo ya hsngani mjini Mtwara

Habari za uhakika zilizoifikia KUSINI zinadai kuwa Murji ambaye alikuwa anatafutwa na polisi tangu jana alimetiwa mbaroni kwa tuhuma za uchochezi katika vurugu za wananchi kupinga gesi kupelekwa dare s Salaam kwa njia ya bomba.

“Tumemwacha maabusu,(Kituo kikuu cha Polisi wilaya ya Mtwara) dhamana wamesema hadi Juma Tatu” kilisema chanzo chetu cha habari

Murji anahusishwana uchochezi kutokana na uwamuzi wake wa kuitisha mkutano wa ndani katika ukumbi wa Kanisa la Pentekosite mjini Mtwara mapema Desemba, 31 mwaka jana na kutangaza kuwaunga wananchi mkono.
Katibu wa Mbunge huyo Mecland Milllanzi amethibitisha kukamtwa kwa bunge huyo na kuongeza kuwa polisi baada ya kumtia mbaroni walifanya upekuzi nyumbani kwake.

Huyo atakuwa kiongozi wa kwanza wa serikali kukamatwa kuhusiana na sakata la gesi, ambapo viongozi wengine ni Katani Katani(CUF) , Uledi Abdallah (NCCR Mageuzi) Saidi Kulaga (CUF ) na Hamza Licheta.
Endelea kufuatilia KUSINI kwa habari zaidi

Advertisements