MTWARA WATAKA SIKU YA UVAMIZI WA WAKOLONI IWE SIKU YA MAOMBELEZO

Suluhisho Nambanga akichangia hoja

Suluhisho Nambanga akichangia hoja

Ahmad Mkumba akichangia hoja

Ahmad Mkumba akichangia hoja

Vijana tunapitia mswada

Vijana tunapitia mswada

Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara limependekeza kuongezwa neno la nchi ya ujmaa na kujitegemea katika rasmu ya Katiba ili kurejesha misingi ya maadili kwa viongozi na watumishi wa umma.

Aidha wajumbe hao wamependekeza kuanzishwa kwa siku za maombelezo kwa tarehe ya kwanza Tanganyika na Zanzibar kutawaliwa kabla ya kusherehekea siku ya uhuru.

Wajumbe hao pia walitaka Katiba ijayo itamkwe wazi kuwa mahojiano ya ajira yatafanyika kwa lugha ya Kiswahili sambamba na mabango na matangazo yote kuandikwa kwa lugha ya kiwasili ili kukienzi.

Akiwasilisha majadiliano ya kundi namba mbili leo lililoangalia sura ya Tatu ya rasmu ya Katiba mpya inayozungumzia maadili na miiko ya uongozi wa umma, Esha Chilonda alisema rasmu walioichambua haizungumzii ujamaa na kujitegemea na kwamba ni muhimu vipenele hivyo vikaingizwa.

“Katiba itamke wazi kuwa hii ni nchi ya ujamaa na kujitegemea, ili turudi kwenye msingi ambayo viongozi wa Taifa waliweza kuzingatia maadili na miiko ya uongozi” alisema Chilonda

Wakichangia hoja mbalimbali za kundi hilo wajumbe pia walipendekeza kuanzishwa kwa siku ya maombelezo kwa kuzingatia tarehe ambazo wakoloni walivamiamataifa hayo kwa mara ya kwanza.

“Sura ya kwanza kifungu cha 3 kinazungumzia siku Kuu za Kitaifa, hapa wameweka siku ya Uhuru, lakini ukiangalia siku ya uhuru kunatolewa historia za majonzi, sasa mimi napendekeza kuwapo kwa siku ya maombelezo ya kuvamiwa kwetu kabla ya huo uhuru” alisema Shaibu Chikoi.

Wakizungumzia Sura ya kwanza kifungu cha 4 kinachoelezea lugha ya Taifa na lugha za alama, wajumbe hao walitaka katiba ijayo iweke wazi kuwa shughuli zote za kitaifa zitaendeshwa kwa lugha hiyo hata kama atakuja mgeni asiyeifahamu.

“Usaili wa kuomba kazi lazima uendeshwe kwalugha ya Kiswahili ili lugha isiwe kikwazo cha kupata ajira, pia mabango yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili, kama mgeni haelewi atatafuta mkalimani…katiba iweke wazi kuwa shughuli zote za kitaifa zitaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili” alisema Ahmad Mkumba

Awali mwenyekiti wa baraza hilo, Fatma Ali aliwataka wajumbe kuwa wazikuchangia nakwamba tume hiyo haina msimamo bali inasikiliza na kuandika maoni ya Watanzania.

Tume hiyo itaendelea kesho na mabaraza ya wilaya katika wilaya ya tandahimba mkoani Mtwara.
Mwisho

Advertisements