GARI LILILOBEBA MABOMBA YA GESI LAVAMIWA

Gari lililobeba mabomba ya gesi likiwa limevunjwa kioo

Gari lililobeba mabomba ya gesi likiwa limevunjwa kioo

942740_658926390802729_1722741960_n

Watu wasiojulikana juzi walivamia gari iliyobeba mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaama na kuvunjaa kioo cha mbele cha gari hilo.

Habari zinasema kuwa tukio hilo limetokea majira ya 11 alfajiri wakati gari hilo likitokea bandari ya Mtwara ambako yamewasili kwa Meli kutoka China kuelekea Lindi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Inadaiwa kuwa likiwa maeneo ya Msijute watu wasiojulika walivamia kwa kurusha mawe gari hilo na kufanikiwa kuvunja kioo cha mbele.

Hata hivyo kamanda wa polisi wa mkoa wa Mtwara Linus Sinzumwa amesema gari hilo halikuvamiwa bali kioo hicho kilivunjika baada ya tairi la mbele la gari hilo kukanyaga jiwe na kuruka kisha kugonga kioo.

“Hakuna uvamizi wowote ni ajali kama ajali nyingine, dereva alikanyaga jiwe na liliporuka lilipasua kioo cha mbele” alisema Sinzumwa

Tukio hilo limetokea siku moja tangu mabomba hayo yawasili mjini Mtwara kutokea China kwa Meli.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni kulitokea vurugu kubwa zilizosababisha watu watau kuuawa na polisi na wengine kujeruhiwa wakipinga mradi huo wa usafirisdhaji wa gesi kwa njia ya bomba.

Mwisho

Advertisements