SHEIKH, WANANCHI WASUSA MASHUJAA MTWARA

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Joseph Simbakali akitoa heshima

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Joseph Simbakali akitoa heshima

Wanajeshi wakipiga risasi hewani

Wanajeshi wakipiga risasi hewani

wakiombeleza silaha begani

wakiombeleza silaha begani

Maombelezo vichwa chini

Maombelezo vichwa chini

Tunatoa heshima

Tunatoa heshima

Simbakalia akizuru makabuli

Simbakalia akizuru makabuli

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Masheikh ‘wamesusa’ kuhudhuria maazimisho ya siku ya Mashujaa nchini ambayo katika mkoa wa Mtwara yalifanyika Makabuli ya Mashujaa wa Vita vya Ukombozi Nchini Msumbi yaliyopo Naliendele mjini hapa.

Hali hiyo ilisababisha kutoombwa kwa dua ya dini ya kiisilamu katika hafla hiyo fupi, hali iliyozua maswali mengi kwa watu waliohudhulia.
Pamoja na hali hiyo mwitikio wa wananchi kushiriki katika maazimisho hayo ulikuwa mdogo, wengi wakidai kuumizwa na kitendo cha baadhi yao kuteswa na wanajeshi hao siku za hivi karibuni kufuatia vurugu za kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam.

Msema chochote katika hafla hiyo alithibitisha kuwa viongozi wa dini hao walialikwa lakini kutokana na sababu hazikufahamika hawakuweza kuhudhuria.

Licha ya jeshi hilo kutoa Mabasi ya kuwapeleka na kuwarudisha wananchi katika eneo hilo la tukio lililopo kilomita Saba kutoka mjini Mtwara, bado raia walisusa maazimisho hayo tofauti na miaka iliyopita.

Advertisements