WADAU WAIPONGEZA UTAFITI NALIENDELE

Picture 006

Dk. Louis Kasuga Mtafiti wa Korosho ARI Naliendele Mtwara

Dk. Louis Kasuga Mtafiti wa Korosho ARI Naliendele Mtwara

Wadau wa tasnia ya Korosho nchini wameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Mazao Naliendele (NARI) mkoani Mtwara kwa kuwezesha upatikani wa teknolojia mbalimbali za uzalishaji bora wa zao hilo hali iliyoongeza uzalishaji na kipato cha wakulima.

Wakichangia mada ya mchango wa sekta ya utafiti katika kuendeleza zao hilo iliyowasilishwa na Dk. Louis Kasuga katika mkutano wa wadau uliofanyika hoteli ya African Dreams mjini Dodoma mwishoni mwa wiki, wajumbe hao walisema taasisi hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa wakulima dhidi ya uzalishaji bora wa zao hilo.

“Naipongeza taasisi ya utafiti Naliendele kwa jitihada zao za kuhakikisha wakulima tunapata teknolojia bora za uzalishaji wa zao hilo, kwangu imekuwa msaada mkubwa kwa sababu nimeweza kuongeza uzalishaji wa zao hili baada ya kupata elimu kutoka kituoni hapo@ alisema Nickodemas Nahonyo mjumbe wa mkutano huo.

Aliongeza kuwa ” Rai yangu kwa sisi wadau kuwezesha taasisi kurekebisha changamoto zinazoikabili ili kituo kiweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi…bila utafiti hakuna kilimo cha kkorosho, huu ni muhimili wetu sisi wakulima wa Korosho”

Awali Dk. Kasuga alisema Taasisi ya Utafiti na Maendeleo ya Mazao Naliendele imeweza kutoa teknolojia mbalimbali za uzalishaji bora wa zao la korosho na kwamba kwa sasa linakabiliwa na changamoto ya kufikisha teknolojia hizo kwa wakulima, sannjari na ufinyu wa bajeti.

“Hadi sasa tunaweza kusema ni asilimia 40 tu ya teknolojia tunazozalisha zimewafikia wakulima wetu, hii ni changamoto kwetu hivyo tunaomba ushirikiano wa wadau katika kuhakikisha teknolojia hizo zinawafikia wakulima na wanazifuata” alisema Dk. Kasuga

Aliongeza kuwa “Pia taasisi inakabiliwa na ufinyu wa bajeti, utafiti ni gharama hivyo kiwango cha fedha tun achopata hakikidhi mahitaji ya utafiti”

Mwisho

Advertisements