MAJI NDANDA YAFUNGIWA

IMG_0921
Maji ya Ndanda Springs pichani

Kiwanda cha Maji cha Ndanda Springs kilichopo kijiji cha Mwena , eneo la Ndanda wilayani Masasi mkoani Mtwara kimefungiwa kuzalisha maji hayo kutokana na madai ya kushuka kwa ubora wake.

Ofisa Afya wa Mkoa wa Mtwara, Jamal Mbava alisema katika ukaguzi uliofanywa Agosti, 12 na 13 mwaka huu wilaya ya Newala mkoani hapa ulibaini uwepo wa takataka zinazoelea na kuonekana kwa macho katika katoni 93 Mussa Kazibure.

Kwa mujibu wa barua ya ofisa huyo kwenda kwa mkurugenzi wa kiwanda hicho ya tarehe 23/09/2013 yenye kumbukumbu Na: RHO/TFDA/5/63 maji hayo kukutwa na takataka ndani ni kukiuka kifungu cha sheria Na 30 (2) cha TFDA

Alisema katoni hizo zikiwa na batch namba tofauti yaani 040912/160812 na 030912 zilikamatwa na kuwekwa katika ofisi ya afya ya wilaya hiyo huku sampuli za maji hayo zikipelekwa kwa mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi.

“ Kwa mamlaka niliyonayo chini ya sheria za Tanzania No. 1 ya chakula, dawana vipodozi ya mwaka 2003 kifungu cha 106 (F), nikaandika na kutoa mari ya kufunga kiwanda hicho mkapa hapo tutakapopata majibu ya kimaabara kutoka TFDA DSM” alisema Mbava

Aliongeza kuwa “ Kwa taarifa hii ambayo naitoa kwenu naomba wananchi kuchukua taadhari wakati wa kutumia maji hayo ya kunywa , popote pale maji hayo yanapofika na pindi wakibaini hasa batch hizo na zinginezo ambao chupa zake zitaonekana kuwa na taka zinazoelea ambazo kitaalamu zinaitwa kwa ujumla kwa jina moja tu la ‘Impurities’ watoetaarifa katika ofisi za afya zilizo karibu yao”

Advertisements