WATANZANIA WENGI HAWAJU KUANDIKA BARUA

Jengo la Posta mjini Mtwara

Jengo la Posta mjini Mtwara

Licha ya kufundishwa shule za msingi uandishi wa barua, imebainika kuwa Watanzania wengi hawajui kuandika barua hadi sasa.

Ofisa Masoko wa Shirika la Posta Mkoa wa Mtwara, Dismasi Nziku alibainisha hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni sehemu za maazimisho ya siku ya Posta Diniani.

Alisema kupitia barua wanazopokea na kuzisafirisha maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi wamebaini kuwa uandishi wa barua ni moja ya tatizo linalowakabili Watanzania wengi.

‘‘Watu wanaweza kujiuliza tumejuaje, wengine watafikiri tunazifungua barua za wateja wetu na kuzisoma, ukweli ni kwamba kupitia uandishi wa anuani zao juu ya bahasha inatupa picha halisi ya uandishi wa barua’’ alisema Nziku

Aliongeza kuwa ‘‘Utakuta anuani imeandikwa wima kwenye bahasha, wengine nyuma ya bahasha…hii ni ishara kuwa hata barua yenyewe haitakidhi viwango…inashangaza kuona hili wakati uandishi wa barua unafundishwa shule ya msingi”

Kwa upande wake Meneja wa shirika hilo mkoa wa Mtwara, Evaristo Mihu amesema kumekuwapo na ongezeko la asilimia 200 la utumaji wa barua mkoani hapa kwa njia ya posta licha ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano kushika kasi.

‘‘Liha ya uwapo wa simu za mkononi na huduma za Internet bado kumekuwapo na ongezeko kubwa la utumaji wa barua kwa njia ya posta…katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka jana tulipokea barua 14190, katika kipindi kama hicho mwaka huu tumepokea barua 45734 sawa na ongezeko la asilimia 200, hizi ni barua za ndani” alisema Mihu

Aliongeza kuwa ‘‘ Barua za nje zimeongezeka kufikia 4000 kutoka 3000 sawa na ongezeko la asilimia 35 … ogezeko hili kwa kiasi kikubwa linatokana na barua za maombi ya kazi, vyuo ambazo zinapitia posta’’

Alibainisha kuwa utumaji pia utumaji kwa njia ya EMS umeongezeka kwa asilimia 31 ndani ya nchi na asilimia 107 nje na kwamba ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano haujaathiri kwa kiwango kikubwa utendaji kazi wa huduma zao.

Advertisements