CCM CHATAKA WAKULIMA KUSIMAMIA MAUZO YA KOROSHO

Shaibu Akwilombe

Shaibu Akwilombe

Abdallah Bakari,

Mtwara.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mtwara kimepingana na Bodi ya Korosho nchini (CBT) juu ya tafsiri ya bei dira ya zao hilo katika msimu 2013/14, huku kikiwataka wakulima wake kuwa makini ili haki na maslahi yao yasiporwe na wajanja wachache.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho kwa waandishi wa habari na kusainiwa na Katibu wa hama hicho mkoani hapa, Shaibu Akwilombe, uwauzi huo wa chama umefikiwa Oktoba, 12 mwaka huu mjini Mtwara.

Alisema halmashauri kuu ya mkoa baada ya kukutana katika kikao kilichofanyia Pentekosite mjini hapa wajumbe walikubaliana kutokubaliana na mwongozo wa mauzo ya korosho uliotolewa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Oktoba, 2013.

Akwilombe katika taarifa yake hiyo alifafanua kuwa kwa mujibu wa tafsiri ya CBT bei dira sio kinga ya bei kwa wakulima wa korosho kitendo alichokidai kinatoa mwanya kwa watendaji wasio waainifu kujinufaisha na zao hilo.

“Bei dira kwa msimu huu ni sh. 1000 kwa kilo, mkulima atalipwa sh. 600 na eti sh.400 zinazosalia katika bei dira hiyo kulipwa kwake kwa mkulima itakuwa majaliwa” alisema Akwilombe

Alifafanua “Tafsiri hii mpya ya matumizi ya bei dira siyo tu inaondoa na kufuta maana sahihi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani iliyokusudiwa ambayo ni kujenga mazingira ya uhakika wa bei kwa mkulima bali inajenga mazingira ya kuwandaa wakulia kudhulumiwa…katika hili tunasema hapana”

Aidha halmashauri hiyo imeiagiza serikali mkoa ihakikishe katika msimu huu mkulima analipwa malipo yake yote ndipo makato yanayotozwa na vyama vya ushirika na halmashauri za wilaya yafuate ili kumlinda mkulima kubeba mzigo wa hasara

“Halmashauri Kuu ya CCM inawataka wakulima kuhakikisha wanakuwa macho na makini ili haki zao na maslahi yao yasiporwe na wajanja wachache’’ ilisema sehemu ya taarifa hiyo yenye kurasa tatu.

Mkurugenzi wa CBT, Juma Mfaume Mkanachapa alisema “Ile pesa ya malipo ya awali sh. 600 anayokopa ni mkulima mwenyewe, ilitakiwa mkulima akusanye korosho zake na kuzikabidhi kwa chama cha ushirika, pale zitakapouzwa afuate fedha zake kwa mujibu wa soko sio bei dira”

Aliongeza kuwa ‘‘Bei dira si bei ya mauzo…mi nadhani mfumo huu ndiyo utaondoa ubadhilifu, tutatangaza bei ya kila mnada, wakulima watajua korosho zao zimeuzwa shilingi ngapi, wizi utatokeaje hapo’’
mwisho

Advertisements