WAWILI WAONGEZEKA KESI YA AL SHABAB MTWARA

Watuhumiwa wa mafunzo ya Al shabab

Watuhumiwa wa mafunzo ya Al shabab


Na Haika Kimaro
Mtwara
Polisi mkoani Mtwara imekamata watu wawili kwa tuhuma za kufanya mafunzo ya Al shababi katika msituni wilayani Nanyumbu mkoani hapa na kufanya idadi ya waliokamatwa kufikia 13.

Watuhumiwa hao kwa pamoja watafikishwa kwa mara ya kwanza na 11 kwa mara ya pili katika Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu leo.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen alisema kuwa wamekamata watu wengine wawili na kufikia idadi ya watu 13 na kwamba uchunguzi unaendelea kwani kuna mambo mengi yanahitaji uchunguzi wa kina.

Kamanda Stephen alisema kuwa watuhumiwa wa mara ya kwanza tayari walikuwa wamefikishwa katika mahakama ya wilaya Nanyumbu na hivyo sasa wanafanya utaratibu ili kesi yao iweze kuhamishiwa mkoa.

“ Idadi ya watu waliokamatwa wakifanya mazoezi ya kigaidi katika wilaya ya Nanyumbu kutokana na vifaa walivyokuwa wakitumia sasa imeongezeka na kufikia 13 baada ya kuwakamata wengine wawili,”alisema Stephen

Aidha kamanda aliongeza kwa kusema kuwa walitegemea kesi ya watuhumiwa hao ingehamishiwa mahakama ya mkoa lakini bado kuna taratibu za kisheria mbazo ni lazima zifuatwe na kwamba wanasheria wako kwenye mchakato kuona sheria zinazotumika zinatizamwa kwa kina kuona ni nini mashtaka yao.

“Tulitegemea kesi yao ingehamia hapa lakini kuna mambo ya kisheria ambayo ni lazima yafuatwe hivyo tukitoka hapa tunaenda kumalizia taratibu ili wahamie huku,haya ni mambo ambayo hayaishi kienyeji ,” alisema
Mwisho.

Advertisements