BALOZI WA FINLAND AZINDUA BLOG YA WAANDISHI MTWARA.

1Na Faraji Feruzi.
Balozi wa Finland hapa nchini Sinikka Antila hii leo ameshiriki katika uzinduzi wa blog ya waandishi wa habari mkoa mtwara wakati akitembelea mabanda mbalimbali katika maonesho ya tamasha la MAKUYA 2013 katika uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara.

Akizindua blog hiyo inayojulikana kwa jina la kusini.wordpress.com akiongozana na kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara Ponsiano Damiano Nyami, balozi Antila amesifu na kupongeza hatua hiyo ya waandishi wa habari mkoa wa Mtwara kwa hatua kubwa waliyofikia ambayo itatanua wigo wa kupashana habari wao kwa wao lakini hata jamii kwa ujumla.

4Amesema kuwa ni nadra kwa waandishi wa habari kuungana na kuanzisha kitu cha pamoja hususani cha kihabari kama hicho, hivyo huo ni mwanzo mzuri na klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mtwara itakuwa imeonyesha njia hata kwa klabu nyingine hapa nchini.

1“Nimefurahishwa na hatua mliyofikia, ni hatua muhimu katika kukuza wigo wa upashanaji habari nawapongeza katika hili” Alisema Balozi Antilla.

Awali katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mtwara,ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa blog hiyo, Abdallah Nassoro alisema uanzishwaji wa blog hiyo unalenga kuboresha huduma za habari kwa kuwafikia watu wa ndani na nje ya nchi kwa urahisi zaidi.

Alisema mtandao huo utatoa habari kwa mujibu wa kanuni, maadili na misingi ya uandishi bora ya habari na kwamba hakutakuwa na tofauti ya kiubora kati ya habari zitakazotolewa na mtandao huo na zile zitakazotolewa na vyombo vya habari vingine.
3
“Mtu atayesoma mtandao huu, ni sawa na yule atakayepata habari kupitia vyombo vingine ikiwemo radio, Televisheni na magazeti katika ubora na umakini wake” alisisitiza katibu huyo.
5

Advertisements