MWANDISHI NYAISANGA AFARIKI DUNIA

Uncle J

Uncle J

Meneja wa Aboud Media, Julius Nyaisanga,ambaye alikuwa mtangazaji wa Radio One Julius Nyaisanga, amefariki dunia leo majira ya saa moja asubuhi katika hospitali ya Mazimbu Mkoani Morogoro.

Taarifa za awali kutoka vyanzo mbalimbali vya habari hususani mitandao ya jamii, na vyombo vya habari, zinasema kuwa marehemu Nyaisanga alikuwa anasumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu pamoja na kisukari.

Wakati wa uhai wake, marehemu Nyaisanga aliwahi kufanya kazi sehemu mbali mbali ikiwemo katika makampuni ya IPP ambako alikuwa mkurugenzi wa Radio One pamoja na Radio Tanzania wakati huo ikiitwa RTD ambako alikuwa mtangazaji wa vipindi mbali mbali. Marehemu ameacha mjane na watoto watatu.Mungu amlaze mahali pema peponi.