CHAUME NA RASILIMALI ZA UMMA

Wakazi wa kata za Luagala, Mnumbwe, Litehu, Chaume, Mkonjowano na Lienje.wilayani Tandahimba wakifuata jambo wakati wa wa mafunzo juu ya namna ya kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma.

Wakazi wa kata za Luagala, Mnumbwe, Litehu, Chaume, Mkonjowano na Lienje.wilayani Tandahimba wakifuata jambo wakati wa wa mafunzo juu ya namna ya kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma.

RASILIMALI ZA UMMA,
Na Kusini Ripota, Chaume.
MAFUNZO ya uwajibikaji wa jamii katika usimamizi wa rasilimali za umma
katika sekta ya kilimo na mifugo yamebaini kuwapo kwa ubadhilifu
uliofanyika katika mradi wa DADPS wa ufugaji wa kuku wa kienyeji uliotekelezwa mwaka 2009/2010, katika kijiji cha Mkwedu kata ya Chaume, Wilaya ya Tandahimba mkoani hapa.
Hayo yalijitokeza katika mafunzo hayo ya siku nne yaliyomalizika
mwishoni mwa wiki, ambayo yaliandaliwa na Shirika lisilo la
kiserikali la Tandahimba Agriculture Development Association (TADO) na
kufadhiliwa na The Foundation For Civil Society (FCS)na kufanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za kata ya Chaume, kijijini hapo.
Ilikuwa ni baada ya mada ya uwajibikaji kwa jamii katika
kushirikishwa katika miradi ambayo inapelekwa katika vijiji vyao, ndipo
alipoamka mwanakijiji wa kijiji cha Mkwedu. Issa Hamisi na
kuulizia hatima ya mradi wa kuku katika kijiji chake, ambapo kwa
mujibu wa maelezo yake ni kwamba haukuelewaka mwisho wake na ulikosa ushirikishwaji wa jamii.

“ Kama ni hivyo mnayotufundisha haya kwamba tunapaswa kuulizia miradi
ambayo inafika vijijini mwetu… basi ningependa kujua mradi wa kuku wa
DADPS ilikuwa hatujaelewa mpaka sasa kwani tulitakiwa kupewa sh.
1,605,000 kwa mujibu wa maelezo ya halmashauri, na fedha hizo ni kwa
ajili ya ujenzi wa banda, kununua kuku, pamoja na chakula cha kuku”
alisema. Hamisi na kuongeza kuwa:
“Lakini tuliishia kupewa sh. 600,000 tu kwa maneno na badala yake
tukapewa sh. 400,000 na hizo zingine sh. 200,000 hutajapewa mpaka leo
hii ambapo tulijenga banda ambalo halikukamilika kwa kukosa milango
na nyaya za madirisha na hivi sasa limetelekezwa kabisa” alisema.
Hamisi.
Hata hivyo ubadhilifu huo ulithibitishwa na katibu wa mtandao wa
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali katika Wilaya ya Tandahimba
(TANGONET).Alli Mchila, alipoomba kutoa ufafanuzi wa miradi hiyo ya
kuku kwani alikuwa mjumbe wa kamati ya ufuatiliaji ambapo alisema
halmashauri ilitenga sh. 35 milioni kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa
kienyeji katika vijiji 20, lakini miradi hiyo kwa asilimia 90
haikukamilika.
“Wanamafunzo ninacho kumbuka ni kwamba mimi nilikuwa mjumbe katika
kamati ya ufuatiliaji ambapo halmashauri ilitenga sh.35 milioni kwa
ajili ya miradi katika vijiji 20 kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa
kienyeji hivyo basi nilishiriki pia katika kufanya tathimini na
ufuatiliaji katika kijiji cha Mwangaza” alisema Mchila na kuongeza
kuwa.
“Matokeo tuliyoyakuta yalikuwa banda lilikuwa tayari limeshabomoka
ambapo idadi ya kuku haikuwa ile iliyotarajiwa kuwepo ilipofikia
wakati huo yaani mwaka 2012 na baya zaidi mahudhurio ya viongozi
pamoja na wana kikundi hayakuwa ya kuridhisha na kutafanya kuwa na
mashaka ya kwamba wamekimbia kuulizwa maswali” alisema katibu huyo wa
mtandao.
Aidha, mwezeshaji wa mafunzo hayo. Aidani Chipande, aliwasifu
wanamafunzo hao kwa kuelewa kwa haraka na kuanza kushughulikia
matatizo ya miradi hata kama imeshapita kwani hiyo ni dalili nzuri
kuwa fedha za wafadhili haziendi bure na wakitoka hapo makubwa
yataenda kufanyika huko vijijini.
“Hii ni dalili nzuri kwamba fedha za wafadhili haziendi bure, kumbe
Inaonyesha kuwa wengi walikuwa hawajui maana ya uwajibikaji katika
rasilimali za umma na ushirikishwaji katika miradi ya jamii vijijini,
sasa mtakwenda kufanya vizuri huko katika maeneo yenu vijijini”
alisema. Chipande.
Mafunzo hayo yalishirikisha maafisa ugani wa
vijiji,wenyeviti wa vijiji,watendaji wa vijiji, wananchi wa kawaida,
taasisi mbalimbali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutoka kata
za Luagala, Mnumbwe, Litehu, Chaume, Mkonjowano na Lienje.
Mwisho.

Advertisements