BIMA YA AFYA YAWABANA WANAOTUMIA KADI BANDIA

Meneja wa mfuko wa bima ya afya nchini NHIF mkoa wa Mtwara. Joyce Sumbwe. akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wa mkoa wa Mtwara kwenye mkutano wa mafunzo ulioandaliwa na mfuko huo  na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa nhif jengo la Posta mjini hapa.

Meneja wa mfuko wa bima ya afya nchini NHIF mkoa wa Mtwara. Joyce Sumbwe. akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wa mkoa wa Mtwara kwenye mkutano wa mafunzo ulioandaliwa na mfuko huo na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa nhif jengo la Posta mjini hapa.


BIMA YA AFYA YAWABANA WANAOTUMIA KADI BANDIA
Na Kusini Ripota, Mtwara.
WANACHAMA wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoani Mtwara wamehimizwa kurejesha kadi zao za uanachama mara baada ya uanachama kufika kikomo ili kuepusha kadi hizo kutumika kwai kufanya hivyo ni kuvunja sheria na atakayebainika kuendelea kutumia atachukuliwa hatua za kisheria.
Hayo yalielezwa juzi na meneja wa mfuko huo mkoa wa Mtwara,Joyce Sumbwe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Mtwara kwenye mkutano wa mafunzo ulioandaliwa na mfuko huo kwa kushirikisha club ya waandishi wa habari mkoani hapa na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa nhif jengo la Posta mjini hapa.
Alisema ofisi yake imebaini kuwapo kwa baadhi ya wanachama ambao ajira zao zimekoma lakini bado wamekuwa wakiendelea kutumia kadi hizo badala ya kuzirejesha kwaajili yao kama sheria inavyoekeleza, ambapo alisema wamebaini hayo kupitia uchunguzi walioufanya katika baadhi ya hospitali na vituo vya afya mkoani hapa.
Sumbwe alisema moja ya wajibu kwa mwanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya ni pamoja na kutambua umuhimu wa kurejesha kitambulisho mara baada ya ukomo wa uanachama wake unapokuwa umefikia, hatua hiyo itasaidia kuvifanya vitambulisho hivyo visiendelee kutumika kwa watu ambao si walengwa katika mfuko huo kwa kuwa kufanya hivyo ni kuusababishia mfuko hasara.
Aidha meneja huyo aliongeza kuwa utambuzi wa mwanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (CHIF) hutambulika kwa kadi ya NHIF katika vituo vya kutolea huduma ambapo kitambulisho cha matibabu hutolewa baada ya kujaza fomu na kuwasilisha katika ofisi ya mfuko huo.
“Tunawaomba hawa wanachama ambao uanachama wao umefika kikomo kuwa na desturi ya kurejesha kitambulisho hii itasaidia kivifanya visiendelee kutimika… sasa hivi kuna baadhi ya watu wanatumia vitambulisho ambavyo wanachama husika uanachama wao umefikia kikomo jambo hili ni kinyume cha sheria,”alisema Sumbwe
Sumbwe alizitaja haki za mwanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya kuwa ni kupata kitambulisho,kupata huduma zote zitolewazo katika kitita cha mafao chini ya utaratibu uliyopo ikiwemo kutoa maoni kuhusu huduma zitolewazo katika vituo pamoja na kutumia maduka ya dawa ya liyosajiliwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
Mkutano huo ulihusisha waandishi kutoka vyombo vyote vya habari venye uwakilishi mkoani hapa, ulilenga kuwajengea uwezo wanahabari ili kutambua shughuli zinazofanywa na mfuko huo, ambapo kwa upande wao wanahabari hao waliupongeza mfuko na kuziomba taasisi nyingine kuiga mfano na kuwaelimisha juu ya shughuli zao ili waweze kuelimisha jamii kwa ufasaha.
Mwisho.

Advertisements