SERIKALI YAOMBWA KUWAPA DILI WAJASIRIAMALI WADOGO

MKURUGENZI mtendaji wa kampuni ya uwkezaji ya Entango, Emma Kawawa akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga mafunzo ya wiki tano kwa wajasiriamali wadogo wanawake yaliyoandaliwa na kampuni yake na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa TTC kawaida mjini hapa (Picha na Hassan Simba).

MKURUGENZI mtendaji wa kampuni ya uwkezaji ya Entango, Emma Kawawa akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga mafunzo ya wiki tano kwa wajasiriamali wadogo wanawake yaliyoandaliwa na kampuni yake na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa TTC kawaida mjini hapa (Picha na Hassan Simba).


WAPENI DILI WAJASIRIAMALI WADOGO WANAWAKE.
Na Ripota wa Kusini, Mtwara.
TAASISI za umma, makampuni binafsi yamehimizwa kuwatumia wajasiriamali wadogo wanawake kuwapa huduma mbalimbali wanazohitaji ili kuwajengea uwezo badala ya kufuata huduma hizo katika makampuni makubwa.
Wito huo umetolewa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Entango. Emma Kawawa, ambayo pamoja na kuwekeza katika masuala ya biashara lakini pia imekuwa ikijuhusisha na kuwainua wajasiriamali wadogo wanaweke kwa kuwajengea uwezo katika nyanja ya elimu na mitaji, wakati akimkaribisha mgeni rasmi kufunga mafunzo ya siku tano ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na kampuni yake.
Emama alisema kuwa ni vema makampuni yanayokuja Mtwara sasa kuwekeza katika nyanja mbalimbali wakawatumia wajasiriamali wadogo wanawake katika kutoa huduma mbalimbali kama chakula, usafi na huduma ya usaidizi katika maofisi yao kwani sasa wameshapata utaalamu wa kutosha katika maeneo hayo.
“Naomba serikali ilione hili hawa wakinamama ambao leo wanahitimu mafunzo ya biashara ya wiki tano wameiva vizuri katika kutoa huduma lugha nzuri na namna ya kuyaweka maeneo yao ya biashara sasa ebu watumieni hawa badala ya kwenda kutafuta huduma kama hizo mbali au ktika makampuni makubwa”, alisema Emma.
Akihutubia katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha ualimu mjini hapa, kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara, Pansiaono Nyami, alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa wajasiriamali wadogo wanawake na hivyo haitawaacha nyumba bali itawashirikisha katika kila jambo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Nyami alisema kuwa serikali katika ngazi zote imekuwa ikiwashirikisha wajasiriamali kwa kuwapa taarifa mbalimbali muhimu kwao pamoja na kuwaunganisha na fursa zinapotokea ili kuwaongezea wateja na hivyo kukuza mitaji yao.
“Na leo hapa nataka nikuambieni kwamba mkuu wetu wa mkoa ambae ndiye aliyenituma kuja hapa kwa niaba yake amesema hivi tena ameongeza haya maneno kwa kuandika kwa mkono kwenye hii hotuba yake ninayoisoma kwenu kuwa iwapo mtaonesha nia ya kuanzisha saccos yenu yenye sura ya kimkoa nitawapa shilingi milioni tano kama kianzio…jamani hii mnaionaje”, alisema Nyami,
Kampuni ya Entango ambayo imejikita katika uwekezaji katika maeneo mbalimbali hapa mkoani imekuwa ikijiuhusisha na kuwainua wajasiriamali wadogo baada ya kufanya utafiti na kubaini kuwa wajasiriamali hao hawana uwezo wa mtaji na elimu ya biashara hali inayowafanya kushindwa kushindana katika biashara na shughuli mbalimbali wanazozifanya.
Mwisho.

Advertisements