Tanecu

MWENYEKITI wa chama kikuu cha ushirika cha wilaya za Tandahimba na Newala, Yusufu Nannila, akitoa taarifa ya makusanyo ya korosho mbele ya waandishi wa habari alipokuwa anaongeanao katika ofisi ya chama hicho mjini Newala juzi.

MWENYEKITI wa chama kikuu cha ushirika cha wilaya za Tandahimba na Newala, Yusufu Nannila, akitoa taarifa ya makusanyo ya korosho mbele ya waandishi wa habari alipokuwa anaongeanao katika ofisi ya chama hicho mjini Newala juzi.


TANECU NA MAKUSANYO YA KOROSHO
JUMLA ya kilo milioni 21,314,157 za korosho zimekusanywa kutoka kwa wakulima wa zao hilo wa wilaya za Newala na Tandahimba mkoani Mtwara tangu kuanza kwa msimu wa mauzo wa 2013/2014. Kwa mfumo wa stakabadhi gharani.
Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika za wilaya za tandahimba na Newala. TANECU, Yusufu Nannila, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake mjini Newala kuwa kiasi hicho kimekusanywa kupitia vyama vya msingi vya wialaya hizo.
Nannila alisema kuwa kati ya korosho hizo zilizokusanywa na kufikishwa katika maghala makuu zilizouzwa kwa mnada kwa wafanyabiashara wakubwa ni kilo 3,201,157 kwa wilaya ya Newala na jumla ya shilingi 5,006,411,483 zilipatikana kutokana na mauzo hayo.
Kwa upande wa wilaya ya Tandahimba Meneja huyo alisema kuwa kiasi kilichokusanywa ni kilo 17,183,467 na fedha zizopatikana kutokana na mauzo hayo ni shilingi 26,750,796,753 na kufanya jumla ya fedha zilizopatikana kwa wilaya zote kuwa shilingi 31,757,208,236 kwa mauzo ya kilo 20,384,644.
“Ndugu yangu taarifa hii ni hadi kufikia Novemba 18 lakini kuna kiasi kingine kimekusanywa na kufikishwa katika maghala makuu…na kesho tutakuwa na mnada kwaajili ya korosho hizo”, alisema Nannila.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa hadi sasa hakuna taarifa ya upotevu wa korosho kwenye maghala makuu wala yale ya vyama vya msingi na kwamba kila kitu kinakwenda vizuri hali ambayo alisema inatia moyo na matumainin kwamba mkulima atapata fedha zake kwa wakati na bila ya kuwapo kwa mapungufu kama ilivyokuwa kwa baadhi ya vyama vya msingi katika msimu uliopita.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amewaonya waendesha maghala na makalani wa vyama vya msingi kuwa makini katika kutunza korosho za wakulima kwa kuzingatia taratibu za mfumo na kwamba upotevu au aina yeyote ya hujuma itakayotokea dhidi ya wakulima haitavumiliwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya atakayehusika.
“Nataka niwaambie watunza maghala na makalani wa vyama vya msingi wawe makini mara hii hatutakuwa na msalie mtume kila atakayehusika namna yayote ya upotevu wa korosho za wakulima huyo hatutamwacha tutahangaikanae hadi tuhakikishe haki ya mkulima inapatikana”, alisema Nannila.
Chini ya mfumo wa mauzo wa stakabadhi ghalani mkulima anakusanya korosho zake katika chama cha msingi kisha zinasafirishwa hadi maghala makuu ambako zinauzwa kwa mnada kisha mkulima anapatiwa malipo yake.
Mwisho.

Advertisements