MIFUKO YA JAMII

MKURUGENZI WA SSRA Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii SSRA. Irene Isaka, akisisitiza jambo wakati akitoa maelezo juu ya kazi za mamlaka hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Mtwara, Willman Kapenjama Ndile kufungua  mafunzo ya siku moja  ya SSRA kwa viongozi wa mkoa wa Mtwara, iliyofanyika leo katika ukumbi wa  Boma mjini Mtwara, ambapo viongozi wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya umma, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na waandishi wa habari walihudhuria

MKURUGENZI WA SSRA
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii SSRA. Irene Isaka, akisisitiza jambo wakati akitoa maelezo juu ya kazi za mamlaka hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Mtwara, Willman Kapenjama Ndile kufungua mafunzo ya siku moja ya SSRA kwa viongozi wa mkoa wa Mtwara, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Boma mjini Mtwara, ambapo viongozi wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya umma, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na waandishi wa habari walihudhuria


KIPATO KIDOGO TATIZO KUJIUNGA MIFUKO YA JAMII.
IMEELEZWA kuwa kipato kidogo miongoni wa jamii ni moja kati ya sababu zinazochangia watu wengi kushindwa kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya jamii nchini na hivyo wengi wao kuishi katika maisha duni zaidi wanapokuwa wazee na kuishiwa nguvu ya kufanyakazi.
Hayo yameelezwa leo na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii SSRA. Irene Isaka, alipokuwa akitoa maelezo juu ya kazi za mamlaka hiyo kwenye mafunzo ya siku moja ya mamlaka yake kwa viongozi wa serikali, mashirika ya umma na wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi wa mkoa wa Mtwara, iliyofanyika katika ukumbi wa Boma mjini hapa.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa watu wengi wanashindwa kuchangia michango ya kila mwezi katika mifuko ya jamii licha ya serikali kuongeza wigo kwa wasio na ajira rasmi kujiunga na kunufaika na mifuko hiyo. Ambapo hata hivyo alisema ni jukumu la kila mfuko kuendelea kuwaelimisha ili waweze kuona umuhimu wa jambo hilo na kujiwekea kidogo wanachokipata kwa maisha yao ya baadae.
Isaka alisema kuwa hadi sasa wanachama wa mifuko ya jamii nchini wamefikia asilimia 1.8 kati ya nguvu kazi yote iliyopo nchini, ambapo michango ya wanachama ni shilingi trioni 1.6 huku mafao yaliyokwishakutolewa yakifikia trion 1.06.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa hadi sasa mifuko ya jamii nchini inahudumia wastaafu 87,000 ambapo vitegauchumi vilivyowekezwa vinafikia thamani ya shilingi trion 4.9 na mali zilizopo zikiwa na thamani ya shilingi trion 6.4.
Akifungua mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya mtwara, willman kapenjama Ndile alisema kuwa tabia ya baadhi ya waajili kushindwa kuwasilisha michango ya watumishi wao katika mifuko ya jamii kwa wakati ni dhuruma na inachangia kuwafanya wafanyakazi hao kuishi maisha mafupi mara baada ya kustaafu.
Ndile alisema kuwa iwapo waajili watakuwa makini na kuwasilisha michango kwa wakati mifuko hiyo itaweza kuwahudumia wanachama wake kwa wakati na hivyo kumuwezesha mstaafu kuendelea kuishi maisha mazuri na marefu kutokana na kuukimbia umasikini kwa kupata mafao yatakayomwezesha kujikimu.
Mwisho.

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Advertisements