stemmuco

MKUU wa wilaya ya Mtwara, Willman Ndile akisisitiza jambo alipokuwa anawasilisha mada katika kongamano la kimataifa la Maadili na Uongozi unaowajibika na madhari ya Kitanzania,lililoandaliwa na taasisi ya Globethics.net lililofanyika katika chuo kikuu cha Stella Maris mjini Mtwara.Ndile aliwasilisha mada iliyohusu Utawala bora uwajibikaji na maadili ya uongozi Tanzania.

MKUU wa wilaya ya Mtwara, Willman Ndile akisisitiza jambo alipokuwa anawasilisha mada katika kongamano la kimataifa la Maadili na Uongozi unaowajibika na madhari ya Kitanzania,lililoandaliwa na taasisi ya Globethics.net lililofanyika katika chuo kikuu cha Stella Maris mjini Mtwara.Ndile aliwasilisha mada iliyohusu Utawala bora uwajibikaji na maadili ya uongozi Tanzania.


MAADILI HAYAPO
IMELEEZEZWA kuwa kukosa kwa maadili kwa baadhi ya viongozi nchini, wasomi kuwa walalamikaji badala ya kushiriki kuleta mabadiliko ni miongoni mwa sababu zinayochangia kuchelewesha maendeleo na kuminywa kwa utawala bora na kutokuwepo kwa uwajibikaji kwa umma.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara, Willman Ndile, alipokuwa anawasilisha mada juu ya utawala bora uwajibikaji na maadili ya uongozi Tanzania katika kongamano la kimataifa la maadili na uongozi unaowajibika lililoandaliwa na taasisi ya Globethics.net, na kufanyika katika chuo kikuu cha Stella Maris mjini Mtwara.
Ndile alisema kuwa viongozi wengi hapa nchini wanaingia katika nafasi hizo kwa rushwa au kujuana na wateuzi wenye mamlaka hali inayowafanya kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na badala yake wanawatumikia waliowateua au kutumia madalaka yao kuchuma mali ili kurejesha fedha walizotoa wakati wanasaka uongozi.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa wasomi wananafasi kubwa ya kubadilisha hali hiyo endapo wataacha kulalamika tu na kuandika maandiko ya kitaalamu inayolenga kuwanufaisha wanaowafadhili badala yake washiriki katika kuleta mabadiliko na kuandika maandiko yenye tija na mwelekeo wa kuibadili mitazamo ya jamii.
Alisema sheria ya maadili inapaswa kufanyiwa mabadiliko ili iweze kuwabana viongozi wengi zaidi badala ya ilivyo sasa ambapo katika ngazi ya wilaya inawahusu viongozi watatu tu huku kukiwa na viongozi wengi wenye mamlaka makubwa na ambayo wengi wao hawayatumii kwa manufaa ya umma na matokeo ni kukosekana kwa uingozi bora ambao ndio nyenzo muhimu kwa utawala bora.
Aidha mkuu Ndile alisema shiria hiyo pia haina maana sana kwani inambana kiongozi kutaja malizake anapoingia lakini haimtaki kutaja mali anapoondoka, lakini pia Ndile alikosoa utaratibu wa baadhi ya watu kumuona fulani ndio mwenye jukumu la kubadili hali mbaya ya kuporomoka kwa maadili na badalayake kila mmoja ajione anajukumu hilo.
Mwisho.