RASILIMALI ZA UMMA

MWENYEKITI wa asasi isiyo ya kiserikali ya Newala Health Improvement Association NEHIA, Hamisi Mawazo akisisitiza jambo wakati anamkaribisha mgeni rasimi kufungua mafunzo ya sikutano ya  uwajibikaji wa jamii katika usimamizi wa rasilimali za umma (SAM/PETS) katika sekta ya afya yanayofadhiliwa na  Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS) yanayoendelea katika ukumbi wa shule ya msingi ya kijiji cha Nandwahi Tarafa ya Kitangali.

MWENYEKITI wa asasi isiyo ya kiserikali ya Newala Health Improvement Association NEHIA, Hamisi Mawazo akisisitiza jambo wakati anamkaribisha mgeni rasimi kufungua mafunzo ya sikutano ya uwajibikaji wa jamii katika usimamizi wa rasilimali za umma (SAM/PETS) katika sekta ya afya yanayofadhiliwa na Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS) yanayoendelea katika ukumbi wa shule ya msingi ya kijiji cha Nandwahi Tarafa ya Kitangali.


ASASI ZITAKAZOKULA FEDHA ZA WAFADHILI KUKIONA
MKUU wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara, Christopher Magalla, ameonya kuwa serikali itazichukuliwa hatua kali za kesheria asasi zisizo za kiserikali zitakazotumia vibaya fedha wanazopewa na wafadhili kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo,
Onyo hilo amelitoa jana wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya uwajibikaji wa jamii katika usimamizi wa rasilimali za umma (SAM/PETS) katika sekta ya afya yanayotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Newala Health Improvement Association NEHIA na kufadhiliwa na Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS) yanayofanyika katika ukumbi wa shule ya msingi ya kijiji cha Nandwahi.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kuwapo kwa asasi zinazoomba fedha kwaajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi na badala yake kuzitumia fedha hizo kwa manufaa yao binafsi kunarudisha nyuma jitihada za serikali na wafadhi katika kuwakwamua wananchi kutoka katika lindi la umasikini na vikwazo vya kiuchumi hivyo serikali haitavumilia hali hiyo.
“Leo tunaona NEHIA wakitimiza wajibu wao kwa mujibu wa mkataba wao na waliowafadhili…huu ni mfano mzuri wa kuigwa na asasi zingine hapa wilayani kwetu na sisi kama serikali tutatoa kilaaina ya msaada utakaohitajika ili mradi huu ukamilike kama ilivyokusudiwa lakini wale watakaotumia vibaya fedha za wafadhili tutawachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafunga jela”, alisema Magalla.
Aidha mkuu huyo wa wilaya ambaye hotuba yake ilisomwa kwa niaba yake na katibu tawala wa wilaya hiyo, Modest Mabula aliwaagiza watendaji wa ngazi zote serikalini wilayani humo kutoa ushirikiano kwa asasi zisizo za kiraia ili ziweze kutimiza malengo yake ikiwa ni pamoja na kuisaidia serikali kutatua matatizo yanayoikabili jamii katika nyanja za uchumi, afya na maeneo mengine.
Kauli hiyo ya mkuu wa wilaya ilikuja baada ya kuelezwa kuwa kuna baadhi ya watendaji serikalini wamekuwa hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa asasi pale wanapoenda kuhitaji msaada wa kiutaalamu ili kutekeleza miradi yao na kutoa kauli za kukatisha tamaa jambo ambalo walidai linazorotesha ushirikiano baina ya asasi na serikali.
Awali akimkaribisha mwenyekiti wa NEHIA, Hamisi Mawazo, alisema kuwa, inatarajia kuendesha mradi wa utoaji wa mafunzo hayo kwa washiriki kutoka katika Kata tano za Nambali, Maputi, Chiwonga, Kitangari na Mtopwa na kujumuisha wahiriki kutoka katika makundi mbalimbali yakiwemo Madiwani, Watendaji wa Vijiji, Watendaji wa Kata, Watumishi wa Sekta ya Afya, Wajumbe wa kamati za Afya, Asasi za Kiraia na wawakilishi wa wanajamii.
“Mheshimiwa mgeni rasmi mradi huu utatekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo awamu ya pili hadi ya nne ni kuunda Kamati ya PETs ambayo itafanya ufuatiliaji ndani ya Tarafa ya Kitangari, kuandaa taarifa ya mradi na kisha kutoa mrejesho kwa wadau mbalimbali katika mikutano itakayoandaliwa na asasi”, alisema Mawazo.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa mada zitakazofudishwa na mtaalamu kutoka mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali wilayani Newala. NEWNGONET Gothard Mwango ni pamoja, dhana ya ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma,ushawishi na utetezi, ufuatiliaji na tathmini kwa miradi mbalimbali ya jamii na mchakato na muundo wa uundaji bajeti.

NEHIA ni Asasi ya Kiraia iliyoanzishwa tarehe 16/08/2010 na kusajiliwa rasmi tarehe 11/04/2011 na Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. ikiwa na lengo kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa Sera mbalimbali za Taifa ikiwamo Afya na linamakazi yake katika kijiji cha Nandwahi wilayani Newala.
Mwisho.

Advertisements