TUMIENI FURSA HII

MBUNGE wa Tandahimba Juma Njwayo akisisitiza jamo alipokuwa anaongea katika mkutano wa hadhara aliouitisha ili kuongea na wananchi katika kijiji cha Nandwani

MBUNGE wa Tandahimba Juma Njwayo akisisitiza jamo alipokuwa anaongea katika mkutano wa hadhara aliouitisha ili kuongea na wananchi katika kijiji cha Nandwani

OLYMPUS DIGITAL CAMERA
TUITUMIE FURSA YA GES ASILIA KUJIIMARISHA KIUCHUMI
WAKAZI wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, wamehimizwa kulima mazao mbadala ya biashara ili kujiongezea kipato badala ya kutegemea korosho pekeyake kwani mazao hayo mengine yana soko la uhakika kutokana na kuwapo kwa wawekezaji wengi wanaowekeza katika sekta ya gesi.
Wito huo umetolewa na mbunge wa Tandahimba juma Njwayo alipokuwa anawahutubia wakazi wa kijiji cha Naputa, ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake ya siku saba kutembelea wananchi vijijini na kufanya mikutano ya hadhara.
Njwayo alisema kuwa kwakuwa sasa mkoni humo imegundulika gesi asilia na wawekezaji wengi wamejitokeza kuwekeza katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda kutokana na kuwapo kwa umeme wa uhakika unaotokana na gesi na biashara nyingine idadi ya watu imeongezeka na mahitaji ya chakula ni makubwa ikilinganishwa na huko nyuma.
“Ndugu zangu hasa nyinyi mnaokaa huku pembezoni mwa mto Ruvuma una fursa kubwa sana ya kuzalisha mbogamboga, matunda na mahindi ya kiangazi ambayo yatapata soko pale mkoani ambao sasa wageni ni wengi na wanahitaji chakula…inashangaza kuona eti nyanya zinatoka Iringa hii ni aibu kwetu tuichangamkie fursa hii ili kujiimarisha kiuchumi”, alisema Njwayo.
Mbunge huyo alisema wilaya imebahatika kuwa na ardhi inayostawi kila aina ya mazao ikiwa ni pamoja na Muhogo, alizeti, mahindi, jamii ya mikunde na mazao mengine ambayo yanaweza pia kuwa mazao ya biashara badala ya kuegemea kwenye korosho pekeyake kwani soko la zao hilo linapoyumba huwa ndio kila kitu kimekwama.
Aidha mbunge huyo aliwahimiza wakazi wa vijiji vyote wilayani humo kujiweka tayari kuupokea umeme kwakuwa tathmini imeshafanyika na vijiji 50 kati ya 157 vitapata umeme katika mwaka wa fedha unaokuja, na kusema kwamba wale watakaokutwa wapo tayari watakuwa wa kwanza kunufaika.
“Jamani umeme sio anasa tena umeme ni maendeleo maana tukiwa na umeme hapa hata nafasi za ajira zitaongezeka kwa kuanzisha viwanda vidogo vya usagaji wa nafaka na usindikaji wa mazao, lakini pia utaturahisishia maisha kwani umeme ukitumika vizuri unaweza kuwa chachu ya maendeleo katika familia zetu”, alisema Njwayo.
Mbunge huyo alisema kuwa maandalizi yanayotakiwa ni kujenga nyumba zilizoezekwa mabati, kujiwekea bajeti ili kuweza kugharimia gharama za uunganishaji wa umeme majumbani, kwakuwa haitakuwa na maana kama serikali itapeleka umeme kijijini kwa gharama kubwa huku wao wakiwa hawapo tayari kuutumia.
Mwisho.

Advertisements