NAZINDUA KIMKOA

OLYMPUS DIGITAL CAMERAMKOA wa Mtwara umezindua dawa ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ijulikanayo kwa jina la Option B+ ambayo mama ataanzishiwa dawa hizo mara tu atakapogundulika kuwa ana maambukizi ya VVU wakati wa ujauzito.

Hayo yameelezwa juzi wilayani Masasi mkoani Mtwara, ambapo mkuu wa mkoa huo Joseph Simbakalia aliwaambia wananchi kupitia hotuba yake iliyosomwa na afisa serikali za mitaa mkoa wa Mtwara ambaye pia ni kaimu katibu tawala wa mkoa huo, Bakari Shamkupa wakati wa hafla ya uzinduzi wa dawa hiyo mpya.

Sherehe hizo ambazo kimkoa zilifanyika wilayani Masasi eneo la uwanja wa fisi kwa kiasi kikubwa zimewezeshwa na wadau wakubwa wanaoshughulika na masuala ya afya ya mama na mtoto mkaoni humoShirika la Elizaberth Glaser Pediatric AIDS Fpundation (EGPAF)kwa kupitia ufadhili wa watu wa Marekani chini ya mashirika yake ya CDC na USAID.

Alisema kuwa madhumuni ya siku hiyo ni kuhamasisha matumizi ya dawa za muda mrefu kwa wanawake wajawazito wenye maambikizi ya virusi vya Ukimwi kwa lengo la kutokomeza maambukizi mapya ya VVU kwa mtoto

Simbakalia alisema ugonjwa wa ukimwi bado ni tatizo kubwa hapa nchini ambalo uathiri watu wa rika zote wakiwemo watoto wachanga kwa kuwa mama mwenye maambikizi ya virusi vya Ukimwi anaweza kumuambikiza mtoto wake wakati ujauzito, uchungu na pindi anaponyonyesha.

“Kila mmoja wetu anawajibu wa kufahamu hali yake ya maambikizi ya virusi vya Ukimwi ili kutambua namna ya kuweza kujinga na kuwakinga na watu wengine ambao hawana hatia hatua hii itasaidia kupunguza maambukizi mapya,”alisema

Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema hatua ya kwanza katika kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto ni kwa mjazito na mwenza wake kujijengea tabia ya kuhudhuria mapema kliniki na kupima kwa pamoja ili kufahamu kama wana maambukizi ya VVU na kwamba iwapo watakundulika ama kutokundulika wataelimishwa.

Alisema kwa mama mwenye virusi vya Ukimwi atazitumia dawa hizo kila siku katika maisha yake yote na kwamba mtoto aliyezaliwa na mama mwenye VVU atapewa dawa hizo kipindi maalumu mara baada ya kuzaliwa ili kumkinga na maambikizi hayo.

Akisoma taarifa ya hali ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi mkoa wa Mtwara mganga mkuu wa mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Mahalifa alisema takrimu za 2012 za mkoa wa Mtwara kwa ujumla inaonyesha kunakiwango cha maambukizi cha asilimia 4.1 katika kipindi cha mwaka 2012.

Alisema akina mama wajawazito wapatao 43,492 walihudhuria katika kliniki ya afya ya uzazi na mtoto na wote hao walipewa huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa VVU na kai ya hao akina mama 877 waliogundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukwimi ambapo ni sawa na asilimia 2.9

Maharifa alisema kuwa katika kipindi cha Junuari 2012 watoto wapatao 745 waliozaliwa na akina mama wenye maambikizi ya virusi vya Ukimwi walifanyiwa kipimo maalumu cha kutambua maambukizi ya VVU kwa watoto wachanga(DNA-PCR) ambapo kati yao watoto 58 sawa na asilimia 5.1walibainika kuwa wameambukizwa virusi vya Ukimwi na mama zao.

Mwisho.

Advertisements