PEMBEJEO ZA RUZUKU

PEMBEJEO ZA RUZUKU
SERIKALI imeuagiza mfuko wa kuendeleza zao la korosho nchini kupatia wakulima wa zao hilo pembejeo za ruzuku kwa wakati unaotakiwa ili kuhudumia mashamba yao kwa wakati sambamba na elimu ya matumizi ya madawa hayo ili waweze kuondokana na matatizo yanayoweza kujitokeza..

Akizungumza na wakulima wa zao hilo kutoka maeneo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa pembejeo za ruzuku msimu wa mwaka 2015/2015 uliofanyika Wilayani Tandahimba jana, mkuu wa Moa wa Mtwara, Kanali Joseph Simbakalia aliutaka mfuko wa kuendeleza zao la korosho nchini kuhakikisha matatizo ya wakulima yanatatuliwa ikiwa ni pamoja na kupatiwa pembejeo za ruzuku kwa wakati.

Kanali Simbakalia alisema kuwa bei ya pembejeo inapopanda serikali imekuwa ikifidia ilipozidi ili kumwezesha mkulima kuipata kwa wakati na hivyo kutaka bei ya ruzuku kuwekwa wazi katika mchanganuo ambao utamwezesha mkulima kuelewa na kutambua mchango wa serikali yao katika kuendeleza kilimo chao kwa lengo la kuinua uchumi.

“Madai ya wakulima ni kwamba hawapati pembejeo kwa wakati, sasa nyinyi mnaweza kufikisha kwa wakati kwa wakala lakini mkulima asiipate kwa wakati, hivyo ni vyema kuhakikisha mtumiaji anaipata kwa wakati unaostahili na bei zikawekwa wazi kwa mchanganu utakaomwezesha mkulima kufahamu alipie kiasi gani,” alisema Kanali Simbakalia.

Mkuu huyo wa mkoa aliwanya mawakalai wasio waaaminifu ambao wamekuwa wakiwauzia wakulima kwa bei ya juu kwamba serikali itawachukulia hatua kali za kisheria ambapo pia aliwataka watendaji wa mfuko huo kushirikiana na wakuu wa wiliya katika kusimamia ugawaji na kuwabaini mawakala wasilio waaminifu.

Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mtendaji Mfuko wa kuendeleza zao la korosho nchini, (CIDTF) Suleimani Lenga alisema kuwa mfuko huo una miaka minne tangu kuanzishwa na majukumu yake ni kuendeleza kilimo cha korosho kwa kusaidiana na bodi ya korosho na pia umekuwa ukigharamia mafunzo ya wakulima na wagani kwa ajili ya utafiti na OLYMPUS DIGITAL CAMERAmadawa.

Aidha Lenga alisema kuwa zoezi la ugawaji wa pembejeo lilishaanza na kwamba mkulima anapaswa kulipa kiasi cha Sh 15,000 kwa mfuko wa kilo 25 ili kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji hiyo ikiwa ni karibu nusu ya bei ya soko ambapo kiasi kingine kimelipiwa na serikali kama ruzuku.

“Lengo la serikali ni kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji hivyo mawakala wahakikishe pembejeo zinamfikia mkulima kwa wakati na kwa gharama iliyopangwa na wakulima wasikubali kununua dawa isiyo ya ruzuku,” alisema Lenga

Mwisho.