WAWAJIBISHENI VIONGOZI WABOVU

KAIMU katibu tawala wa wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara. Salum Palangyo, akisisitiza jambo alipokuwa anawasilisha mada juu ya utawala bora  katika mdahalo wa kuelimisha wakazi wa wilaya hiyo juu  mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya kijiji cha Nanyumbu.

KAIMU katibu tawala wa wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara. Salum Palangyo, akisisitiza jambo alipokuwa anawasilisha mada juu ya utawala bora katika mdahalo wa kuelimisha wakazi wa wilaya hiyo juu mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya kijiji cha Nanyumbu.


WAWAJIBISHENI VIONGOZI WAZEMBE
VIONGOZI wa vijiji, kata na wilaya wameaswa kuitisha vikao vya kisheria kwa wakati ili kutoa taarifa juu ya hali ya mambo yanavyoendelea na hivyo kujenga imani na wananchi wanaowaongoza au kuwawakilisha katika vyombo vya juu na wanaposhindwa kufanya hivyo wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
Hayo yamesemwa juzi kaimu katibu tawala wa wilaya ya Nanyumbu, Salumu Palangyo, alipokuwa anatoa mada juu utawala bora katika mdahalo wa mchakato wa katiba, ambapo alisema ni wajibu wa viongozi kutoa mrejesho kwa wananchi wanaowaongoza na kushindwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na utawala bora.
Katika mdahalo huo ulioandaliwa na mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa Mtwara, MRENGO na kufadhiliwa na The foundation for civil society, ulijumuisha makundi mbalimbali yakiwemo ya walemavu, wastaafu, wajane, vijana walioko shuleni, vijiweni na madiwani na viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa ulifanyika katika viwanja vya ofisi ya serikali ya kijiji cha Nanyumbu.
Kaimu katibu tawala huyo aliwakumbusha viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa kuwa ni wajibu wao kutoa mrejesho kwa wanaowawakilisha kwa kufanya mikutano au kutoa taarifa katika mbao za matangazo kwenye maeneo ya wazi yanayokiwa kwa urahisi na watu wote.
“Ni wajibu wa viongozi kutoa mrejesho kwa wanaowaongoza…wewe kama ni diwani au mbunge usipokuwa na utaratibu wa kutoa mrejesho maana yake hutakuwa mwakilishi wa watu…kwa upande wa vijiji mnatakiwa kufanya mikutano kila baada ya miezi mitatu na kabla hujaenda kwenye vikao unatakiwa kupata maoni ya watu wako na unaporejea pia wape kile kilichotokea kule”, alisema Palangyo.
Aidha Palangyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria alibainisha kuwa wananchi nao kwa upande wao wanawajibu wa kuhudhuria vikao na mikutano inayowahusu, na kuwaeleza kuwa wanapokuwa katika mikutano hiyo wana haki ya kuhoji na kupatiwa ufafanuzi juu ya masuala ya fedha na miradi inayoendeshwa katika maeneo yao.
“Kuna watu wengi ambao huwa hawana tabia ya kuhudhuria mikutano sasa hili ni tatizo ni wajibu wenu kuhudhuria maana pale ndipo mtakapopata nafasi ya kujua nini kinaendelea na pale ambapo hamutakuwa mmeelewa basi mtauliza maswali na viongozi wenu wanawajibika kujibu”, alisema Mwanasheria huyo.
Alisema kuwa wananchi wananafasi kubwa katika dhana ya utawala bora kwano wao ndio wanaowachagua viongozi na kuwaweka madarakani hivyo wanatakiwa kuwa makini katika kufanya uchaguzi ili wasiwaweke viongozi wabovu watakaochelewesha maendeleo na kuzua migokichangia mada hiyo Nicolus Pai kutoka kijiji cha Sengenya, alisema kutoitishwa kwa mikutano na boro isiyo ya lazima.
“Watu kujichukulia sheria mikononi na kuwazomea viongozi wao ni dalili ya kushindwa kwa viongozi kuwajibika katika maeneo yao…lakini hiyo sio njia sahihi mnachotakiwa kufanya ni kuwaondoa madarakani kwa kufuata utaratibu wa kisheria uliowekwa…utashangaza unakuwa wakwanza kuzomea viongozi lakini unapofika wakati wa uchaguzi hujitokezi”, alisema Palangyo.
Mdahalo huo uliohusisha wananchi kutoka tarafa ya Nanyumbu, ulitawaliwa na mada za mabadiliko ya tabia nchi, masuala ya jinsia, utawala bora, uwazi na uwajibikaji pamoja na mabadiliko ya tabianchi, kwa pamoja ulimalizika kwa wananchi kukubaliana kuwa na mabadiliko ya kifikra katika ushiriki wao kwenye vikao vya kupanga maendeleo yao na kwapamoja kuwawajibisha viongozi wazembe kwa kufuata utaratibu uliopo.

Advertisements