WATIMUENI KWA ADABU VIONGOZI WENU

MWEZESHAJI. Francis Mkuti, akisisitiza jambo wakati akitoa mada juu ya utawala bora kwa wakazi wa kijiji cha Namtimbuka katika wilaya ya Mtwara, ambapo aliwaasa wananchi kuacha tabia ya kuwatimua hovyo viongozi wao na badala yake wafuate utaratibu wa sheria na kanuni zilizopo.

MWEZESHAJI. Francis Mkuti, akisisitiza jambo wakati akitoa mada juu ya utawala bora kwa wakazi wa kijiji cha Namtimbuka katika wilaya ya Mtwara, ambapo aliwaasa wananchi kuacha tabia ya kuwatimua hovyo viongozi wao na badala yake wafuate utaratibu wa sheria na kanuni zilizopo.


MSIWATIMUE HOVYO VIONGOZI WENU
WAKAZI wa vijiji vya kata na tarafa ya Nanyamba wilaya ya Mtwara mkoani hapa, wameaswa kutowatimua madarakani viongozi wao wa vijiji na vitongoji au kuwazomea mbele ya viongozi wa juu kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria na ni kwenda kinyume na dhana ya utawala bora.
Wito huo umetolewa juzi na mwezeshaji wa mafunzo ya utawala bora, Francis Mkuti. kwa nyakati tofauti alipokuwa anatoa mada ya utawala bora kwa wakazi na viongozi wa vijiji vya, Namtimbuka, kitamabonden, Mnyahi, Mwang’anga na Chikwaya katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara, ambapo alisema tabia ya wananchi kuwazomea au kuwatimua viongozi wao madarakani bila kufuata utaratibu ni kinyume na dhana ya utawala bora.
Mkuti ambae pia ni afisa wa tarafa ya Ziwani wilayani humo, alisema kuwa katika siku za hivi karibuni kumeibuka mtindo kwa wananchi kuwaondoa madarakani viongozi wao ama kuashindikiza wajiuzuru kabla ya muda wao wa uongozi kupita kwa kisingizio cha viongozi hao kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo au kutowajibika.
“Ndugu zangu wananakijiji na viongozi wenzangu nataka nikuambieni hapa leo kwamba ni vema tunapopoteza imani na viongozi wetu tukawaondoa madarakani kwa kufuata utaratibu wa kisheria na taratibu zilizopo na sio kujichukulia sheria mkono na kuanza kuwazomea na kuhalibu mali zao”, alisema Mkuti alipokuw katika kijiji cha Kitama bondeni.
Akiwasilisha mada ya namna ya kukuwajibisha viongozi alipokuwa katika kijiji cha Mwang’anga, Mkuti alisema kuwa licha ya viongozi wengi wa vitongoji na vijiji kutoitisha mikutano kwa wakati kwa mujibu wa sheria lakini si jukumu la wananchi kuwavamia kuhalibu mali zao au kuwazomea kwani kufanya hivyo ni kinyume na utaratibu.
“Ni kweli viongozi wetu wa vijiji wanaudhaifu mkubwa hasa katika kuitisha vikao na wananchi lakini sio jukumu lako sasa kumtukana au kumzomea…wengine wanafika mbali wanawatuhumu viongozi wao kwa wizi na kuanza kuvamia mali zao kuzihalibu eti zimetokana na pesa za kijiji walizoiba hivi unauhakika gani na jambo hilo kwani mahakama si zipo kama kaiba atahukumiwa na mahakama”, alisisitiza Mkuti.
Akimkaribisha mwezeshaji huyo kutoa mada katika mikutano hiyo, katibu mtendaji wa shirika la saidia jamii kuishi SAJAKU, Nashiri Pontiya ambaye shirika lake ndio lililoandaa mafunzo hayo, alisema kuwa walifikia uamuzi wa kuandika mradi huo baada ya kufanya utafiti na kubaini kuwapo kwa mapungufu makubwa ya kiutawala na masuala ya utawala bora.
Alisema kuwa mafunzo hayo yaliyofadhiliwa naThe foundation for civicil sociaty, yalianza kwa kutoa elimu ya utawala bora kwa viongozi wa vijiji, vitongoji na kata na baadae wananchi wa kawaida na hatua ya sasa ni mikutano ya wananchi na viongozi wao kujadiliana kwa pamoja juu ya masuala ya utawala bora na pale penye mapungufu kutafuta ufumbuzi wake.
“Sisi kabla ya kuandika mradi huu na kuuombe fedha tulifanya utafiti na kubaini kuwa makundi yote ya viongozi na hata wananchi hawana uelewa wa kutosha juu ya dhana ya utawala bora…tunashukuru sasa tumepata huyu mfadhili na kama mnavyoona leo mnapata hii elimu ambayo tunahakika itasaidia kujenga demokrasia na utawala bora katika maeneo yetu”, alisema Pomtiya ambaye pia ndio mratibu wa mradi huo.
Pontiya, alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo viongozi na wananchi katika kutekeleza dhana ya utawala bora na kujenga mahusiano bora ya kiutendaji kati ya watendaji na viongozi wa kuchaguliwa ambapo pia aliyataja maeneo yatakayohusika kuwa ni kata kumi za Nanguruwe,Chawi,Mahurunga, Naumbu, Mbawala,Nanyamba, Njengwa, Kitaya,Kilomba,Mtiniko,Mbembaleo,Nitekela, Milango minne na Namtumbuka.
“Mwisho wa mradi huu tunataka tuone wananchi wakihudhuria katika mikutano huku viongozi nao wakitimiza wajibu wao kwa kuitisha mikutano kwa mujibu wa sheria na miongozo iliyopo”, alisema Pontiya ambaye pia ni mratibu wa mradi huo.
Mwisho.