SHIKAMANENI KATIKA UMOJA

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

SHIKAMANANI KATIKA UMOJA

 

WANACCM wilayani kupitia jumuiya zote za chama hicho Newala mkoa wa Mtwara wameshauriwa kuwa na umoja na  kushirikiana na kuwa na upendo miongoni mwao ili kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo katika chaguzi za serikali zijazo.

 

Wito huo ulitolewa jana na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Newala, Ally Lilama wakati akihutubia katika sherehe za kusimikwa kwa kamanda mpya wa uvccm wilaya hiyo, Fatma Machinga pamoja na naibu wake, Haji Mnasi na makamanda wa kata 28 kutoka katika kata zote za wilaya hiyo.

 

Lilama alisema alisema kuwa mipasuko ndani ya chama ndiyo inayopelekea kuanguka kwa chama na kukosa ushindi hivyo kuwataka kujifunza kutokana na makosa na kujenga misingi imara na kujirekebisha ili pale walipopoteza nafasi katika chaguzi zilizopita wahakikishe safari hii wanashinda.

 

“ Mipasuko ndani ya chama ndiyo inayoyotupeleka pabaya ni vyema tukawa na umoja, upendo na ushirikiana na hakika kwa kufannya hivi tutapata ushindi wa kishindo ila kama ikiwa tofauti ndio tutawapa wapinzani nafasi,” alisema Lilama.

Hata hivyo aliwataka wana CCM kutokupoteza muda wao kwenye majukwaa kwa kuwazungumzia wapinzani na badala yake watumie muda mwingi kuelimisha wananchi juu ya mambo yaliyokwishafanyika na serikali iliyopo madarakani kwani kwa kufanya hivyo watakuwa na nafasi kubwa ya kupata ushindi wa kishindo kwakuwa wapigakura watakuwa wanajua nini kimefanyika.

 

Akihutubia wanaccm muda mfupi baada ya kuapishwa kushika nafasi ya kamanda wa vijana wa wilaya hiyo, Fatma Machinga alisema kuwa atahakikisha anawaongoza vijana kuwa na mshikamano miongoni mwao ili kuhakikisha chama kinakuwa na msimamo unaojenga misingi ya ushindi.

 

Machinga alisema kwakuwa vijana ndio tegemeo kubwa la ushindi wa ccm na kwakuwa vijana ndio nguvukazi na rasilimali muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa nchi atahakikisha vijana wa Newala wanakuwa na shughuli za uzalishaji kipato ili waweze kujitegemea kiuchumi.

 

“Leo nimeapishwa kuwa kamanda wenu nataka nikuhakikishieni wazi kwamba mimi nimjasiriamali nitahakikisha nakuambukizeni ujasiriamali ili muweze kujitegemea maana kama hamutakuwa imara kiuchumi ni rahisi kurubuniwa na kujiingiza katika makundi ambayo hayana tija kwenu na kwa nchi yetu:, alisema Machinga.

 

Akiongea katika halfa hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Umoja mjini Newala, katibu wa uvccm mkoa wa Mtwara. joyce Mwenda alitoa angalizo kwa makanda waliochaguliwa kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia misingi, kanuni na maelekezo ya chama na si kuvuruga vijana na kuwafanya viongozi waliopo madarakani wakashindwa kutimiza wajibu wao.

 

“Najua hapa leo tumewaapisha makanda wa kata na wa wilaya sasa jukumu lenu ni kutulea sisi vijana msiende kuwavuruga madiwani wetu au mbunge wetu mkatumia nafasi hii kujinufaisha binafsi kwa malengo yenu ya kutaka kuwania nafasi hizo subirini wakati ufike”, alisema Mwenda.

Mwisho.

 

Advertisements