VIJANA MTWARA WACHANGAMKIA FURSA

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

ZOEZI la uchukuaji fomu kwaajili ya vijana mbalimbali kushiriki katika Shindano la Mashujaa wa Kesho la Statoil limeendelea kushika kasi huku idadi kubwa ya vijana wakiendelea kurejesha fomu kwa lengo la kushiriki katika kinyang’anyiro hicho.

 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, AfisaMawasilianowa Statoil Tanzania, Erick Mchome alisema hadi sasa zaidi yavijana 150 tayari wamerejesha fomu zao tayari kwa kuyashindanisha mawazo anuai ya miradi yao walio iwasilisha kwaajili ya kushiriki katika shindano hilo.

 

Mchome alisema vijana hao wamejaza fomu kwaajili ya kushiriki katika shindano hilo kuwania kitita cha Dola 5,000 kwa mshindi wa kwanza”.

 

“Kimsingizoezihili la shindano la Mashujaa wa Kesho limepokelewa vizuri na linaendelea vizuri sana vijana wengi wa Mtwara wamejitokeza kuchukua fomu na baadhi wameanza kuzirejesha fomu zao…zaidi ya vijana 150 tayari wamerejesha fomu,” alisema Mchome.

 

Hata hivyo kiongozi huyo aliwataka vijana ambao wamechukua fomu kuzirejesha fomu zao kwa wakati kwenye vituo walivyoelekezwa ili hatua zingine zautaratibu washindano hilo ziweze kuendelea.

 

“NingependakuwakumbushawashirikikuwamwishowakurejeshafomuniOktoba 10, 2014 saa nane kamili kwenye vyuo vya Naliendele Agricultural Institute, Tanzania Institute of Accountancy, VETA, Chuo cha Utumishi na Chuo cha Stella Maris Pamojana Pride FM,” alisisitizaMchome.

 

Akifafanua zaidi, Mchome alisema mchujo wa kupata washiriki 40 watakaoingia hatua ya pili utafanyika mara baada ya zoezi la urejeshwaji fomu kukamilika na kutakuwa na mchujo wa tatu ambao ni wamwisho na kuwato awashindi watano watakao wania dola 5,000 kwa mshindi wa kwanza nadola 1,000 kwawashindi wapili, tatu, na wanne

 

Shindano hilo la vijana linalojulikana kama Mashujaa wa Kesho lenye lengo la kuhamasisha ujasiriamali lilizinduliwa rasmi Septemba 3, 2014 na kampuni ya Statoil na linatarajiwa kumalizikaDesemba 12 mwaka huu.

Reply Forward
Advertisements