Masasi, Nanyumbu wapongezwa ujenzi wa maabara

LUANDA4

SERIKALI mkoan Mtwara imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa agizo la Raisi kikwete juu ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za kata, hasa katika wilaya za Masasi, Nanyumbu na masasi mjini.

Akiongea na watendaji na wataalamu wa wilaya hizo katika kijiji cha Mpindimbi wilayani Masasi mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea na kujionea ujenzi wa maabara katika shule zote za wilaya hizo, katibu tawala wa mkoa huo Alfred Luanda, alisema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa hadi sasa.

Luanda alisema kuwa ingawa bado maabara hizo hazijakamilika lakini ni imani yake kwamba zitakamilika mapema mwezi ujao, hasa kutikana na mwitikio aliouona kwa wananchi na watendaji katika shule alizozitembelea katika ziara yake ya siku mbili iliyomalizika jana.

Katibu tawala huyo alisema kuwa kwa upande wa wilaya ya Masasi karibu maabara zote tisa alizozitembelea alikuta mafundi wapo eneo la ujenzi na mengi kati ya hayo yamefikia hatua ya kupauwa jambo ambalo limemtia moyo na kujiridhisha kwamba lengo litafikiwa.

“Nataka niwatie moyo kazi nzuri na nimeipenda yapo mambo machache ambayo sikuyapenda na hayo nataka myarekebishe mapema kama nilivyotoa maelekeozo tulipokuwa maeneo ya ujenzi…lakini kazi nuri”, alisema Luanda.

Kwa upande wa wilaya ya Nanyumbu katibu tawala huyo pia aliridhishwa na hatua licha ya kuchelewa kuanza kutekelezwa kwa agizo hilo, lakini kasi ya utekelezaji imekuwa kubwa na katika kila eneo alilopita alikuta kazi zikiendelea kwa kasi nzuri.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo wilayani kwake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Masasi, Beatrice Dominic, alisema kuwa wilaya yake inajumla ya shule 26 ambazo zinahitaji maabara 78 lakini baadhi ya shule tayari zinamaabara angalau moja.

Alisema ili kuhakikisha shule zote zinakuwa na maabara tatu kwa kila shule watendaji wamejipanga kwa kushirikiana na wananchi kujenga maabara hizo na kudai kuwa hadi kufikia mwishoni mwa Novemba zitakuwa zimekamilika.

Naye kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya nanyumbu, mhandisi.Davascar Tembo alisema kuwa maabara zinazojengwa katika shule zote za sekondari wilayani humo zinajengwa na mafundi wa maeneo husika chini ya usimamizi wa kamati za ujenzi huku kila mkuu wa idara akikabidhiwa shule moja kuwa mlezi na msimamizi wa karibu wa ujenzi.

Akiwa wilayani Masasi Katibu tawla alitembelea miradi ya ujenzi ya maabara ya shule za sekondari za mpindimbi, Isdore Shirima,Mkalapa, Chanikanguo na Mbembaleo, wakati katika halmashauri ya masasi mjini alitembelea shule za Sululu,Marika na Anna Abdallah.

Akiwa wilayani Nanyumbu mtendaji huyo alitembelea shule za Napacho,Chipuputa,Nangomba,Mikangaula,Sengenya, Likokona, Lumesule na Michiga.

Mwisho.